Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Julai 22, 2024 amefanya Kikao Kazi na Kamati za Usalama za Mikoa na Wilaya Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi wa ngazi ya Mikoa.
Mheshimiwa Majaliwa amefanya kikao hicho kwa njia ya mtandao akiwa Ofisi Ndogo za Waziri Mkuu Magogoni Jijini Dar es Salaam.
Viongozi wa Mkoa wa Arusha wamehudhuria kikao hicho kilichofanyika kwa njia ya mtandao ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Kaganda pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu J. Makwinya wameshiriki kikao hicho na Viongozi wengine kutoka Wilaya ya Arumeru.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa