Kamati ya Siasa Wilaya ya Kichama ya Meru imekamilisha ziara yake kwa siku ya kwanza ambapo imetembelea miradi ya Sekta za Afya, Elimu na Uchumi na Uzalishaji Mali.
Kamati imepongeza utekelezaji wa Ilani katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru na kutoa Maagizo ikiwemo wataalam kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha ya ujasiriamali kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu vinavyonufaika na mikopo isiyo na riba inayotolewa na Halmashauri. Kamati imetoa rai kwa Vikundi kutumia fursa hiyo kujikwamua kiuchumi.
Aidha, Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu vimehamasishwa kutumia mikopo kujiletea maendeleo na kuhakikisha vinarejesha mikopo ili Wananchi wengine waweze kunufaika.
Kamati imewataka Watumishi wa Afya kuhakikisha wanatunza nyumba zilizojengwa na Serikali ili ziweze kutumika kwa muda mrefu.
Aidha, Wataalam wa ujenzi wa Halmashauri wamepewa maelekezo kuhakikisha kuwa wanafanyq ukaguzi wa mara kwa mara wa majengo yote hata yale yaliyokamilika ili kuendelea kutoa ushauri katika ukarabati na utunzaji wake.
Kamati ya Siasa imetoa Wito kwa Wataalam wa Sekta ya Afya kuwahudumia wananchi kwa weledi, kwani sekta ya Afya ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa na kusisitiza ushirikiano kati ya Watendaji wa Kata na Waheshimiwa Madiwani katika kuwaletea Wananchi maendeleo
Katika siku ya kwanza Kamati ya Siasa imetembelea miradi ya ujenzi wa chumba cha maabara katika zahanati ya Kimundo, ujenzi wa nyumba ya mtumishi katika zahanati za Mulala na Kilinga, Kumtembelea vikundi vya Wanawake vya Tikusare na Shukuru, kukagua ujenzi wa Vyumba vya madarasa katika Shule za Msingi Kilimani, Kikatiti na Kitefu .
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa