Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango amekabidhi rasmi Ofisi kwa Mkuu mpya wa Wilaya ya Arumeru Mhe.Emmanuela M. Kaganda.
Mhandisi Ruyango amewashukuru Viongozi wa Halmashauri za Arusha na Meru, Kamati ya ulinzi na Usalama, Watumishi wa Wilaya hiyo, Viongozi wa Dini na Mila na Wananchi kwa Ushirikiano waliompa kipindi cha uongozi wake na kuwataka kushirikiana na Mhe.Emmanuela
Kwa upande wake Mhe.Emmanuela Kaganda, Mkuu mpya wa Wilaya ya Arumeru ametoa dira ya uongozi wa Wilaya hiyo kuwa, utajikita katika ushirikiano na utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa ufanisi mkubwa ikiwa ni pamoja na utoaji wa huduma bora kwa wananchi, ambapo ametoa wito kwa watumishi wote wa umma kutekeleza wajibu wao ipasavyo.
Aidha, Mhe. Kaganda amehimiza kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kuwaletea wananchi maendeleo nchini, hivyo ametoa rai kwa watumishi kutekeleza wajibu wao ipasavyo na kwa matendo.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa