• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

DC ARUMERU ATOA SIKU 1 4 WAVAAMIZI SHAMBA LA SHAMBA LA VALESKA KUPISHA SHUGHULI ZA KITAALAMU

Imewekwa: November 18th, 2021

Mkuu Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango ametoa siku 14 kwa wote waliovaamia Shamba la Valeska lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Meru kupisha taratibu za kitaalamu katika Shamba hilo ambalo awali lilikuwa likimilikiwa na Arusha Cooperative union limited (ACU) , ambapo Mwaka 2008 Serikali   ilifuta  umiliki wake kutokana na ACU kushindwa kuliendeleza .


Mhe. Ruyango ametoa agizo hilo baada ya kuzungumza na wananchi wa Vijiji Vitatu vinavyozunguka Shamba hilo vya  Maroroni, kwaugoro na Valeska ambavyo kila kimoja  kimepewa Ekari 500 kutoka Shamba hilo lenye ukubwa wa Ekari 4087  lililofutiwa umiliki na Serikali  kwa maslahi mapana ya taifa, ambapo  Halmashauri  ya Meru ilipewa jukumu la  kuligawanya  kwa kuzingatia maelekezo yaliyotolewa.

Kesia  Kaaya ambaye ni mkazi wa kijiji Cha Valeska ameishukuru Serikali kwa kutoa Ekari 500 kwani zitasaidia kupunguza uhitaji wa Ardhi "japo Ekari 500 hazitoshi tunaishukuru Serikali kwani tunachangamoto ya ufinyu wa Ardhi, wengi hatuna makazi pia tunaitaji maeneo ya huduma za jamii na ardhi ya vijana kujiajiri kwenye kilimo cha mbogamboga "amesema Kesia

Nao Wananchi waliovaamia Shamba hilo kwa kujishughulisha na kilimo cha mbogamboga  wamesema hawana budi kufuata maagizo ya Serikali japo hawakutarajia kuondolewa kwa muda  uliotolewa "kwa sasa najishughulisha na kilimo cha pilipili  katika Shamba hili" amesema Reward Komba

Nao Waheshimiwa Madiwani wa Kata ya Maroroni na Makiba, ambao  Kata zao zina  Vijiji vilivyopewa Ekari 500 wametoa wito kwa Wananchi kuwa watulivu wakati taratibu za kitaalum ikiwemo upimaji zikiendelea katika Shamba hilo

Ikumbukwe, tarehe Mosi Julai 2021 Mhe.Wilium Lukuvi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi alifanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru na kutoa maelekezo ya Serikali juu ya upangaji wa Shamba la Valeska ikiwa ni pamoja na kuelekeza Vijiji Vitatu vinavyozunguka Shamba Hilo kupewa Ekari 1,500 kwa mgawanyo wa Ekari 500 kwa kila kijiji.

Baadhi ya picha za tukio.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango akizungumza na Wanakijiji wa Kijiji cha Maroroni na kwaUgoro.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru ,Mwl.Zainabu Makwinya wakati wa Ziara ya Mhe.Mkuu wa Wilaya Kata ya Maroroni.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru akizungumza na wananchi wa Maroroni.

Baadhi ya Wanakijiji wa Kijiji chaValeska wakifuatilia Mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.

Baadhi ya Wanakijiji wa Kijiji chaValeska wakifuatilia Mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.

Baadhi ya Wanakijiji wa Kijiji chaValeska wakifuatilia Mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.

Baadhi ya Wanakijiji wa Vijiji vya Maroroni na kwaugoro wakifuatilia Mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.

Baadhi ya Wanakijiji wa Vijiji vya Maroroni na kwaugoro wakifuatilia Mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.

Baadhi ya Wanakijiji wa Vijiji vya Maroroni na kwaugoro wakifuatilia Mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.

Baadhi ya Wanakijiji wa Vijiji vya Maroroni na kwaugoro wakifuatilia Mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.

Baadhi ya Wanakijiji wa Vijiji vya Maroroni na kwaugoro wakifuatilia Mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.

Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • MAADHIMISHO WIKI YA UTYUMISHI WA UMMA 2025 DODOMA

    June 13, 2025
  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa