• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

DED MERU AHAMASISHA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWENYE DIWANI CUP

Imewekwa: October 6th, 2024

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu J. Makwinya ambaye pia ni Msimamizi wa Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa ameshiriki kama Mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Amir Mkalipa katika Ligi ya Mpira wa Miguu iliyoandaliwa na Diwani wa Kata ya Uwiro Mhe. Dauson Urio, Ligi  iliyopewa jina la DIWANI CUP.

Ligi ya DIWANI CUP iliyofanyika leo tarehe 06 Oktoba,2024 ikiwa na lengo la kukuza  michezo na  kuhamasisha Wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye Daftari la Wakazi la wapiga Kura pamoja na kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Mkurugenzi Mtendaji na Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Makwinya amepata fursa kutoa elimu kwa wananchi wa Kata ya Uwiro kuhusu  uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa kwa ngazi ya Mtaa na Kijiji pamoja na kueleza sifa za Kugombea na Kupiga Kura kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Mbali ya kutoa elimu hiyo, Msimamizi wa Uchaguzi  na Afisa Uchaguzi Ndg. Edward Bujune wamegawa vipeperushi  kwa wananchi vyenye maelezo yanayohusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa vikionyesha sifa za wagombea na wapiga kura pamoja na tarehe za kujiandikisha na tarehe ya Uchaguzi.

Hata hivyo, Katika uhamasishaji huo uliofanyika katika Kata ya Uwiro wananchi wamepatiwa elimu ya utofauti wa kujiandikisha kwenye daftari la Wakazi na Vitambulisho vya Kura vitakavyotumika kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwakani 2025.

Timu zilizoshiriki katika mashindano ya fainali ya DIWANI CUP ni Timu ya Kivumbi na Timu ya Kimulimuli ambapo  Timu ya Kimulimuli imeibuka Kidedea kwa mikwaju ya Penati goli 4-3  baada ya Mchuano mkali wa dakika 90 bila kufungana.

Mhe.Diwani Kata ya Uwiro Dauson Urio kwa niaba ya Wananchi wa Kata ya Uwiro yenye vijiji vitatu vya Kisimiri Juu, Kisimiri Chini na Uwiro ametoa shukrani kwa Mkurugenzi Mtendaji kwa kufika na kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

"Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze kushiriki Uchaguzi"


Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • TAHAPAO NA MERU DC WAWEKA NGUVU KWENYE KAMATI ZA MTAKUWA

    February 19, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa