HALMASHAURI YA WILAYA YA MERU YAKABIDHI PIKIPIKI KUMI ZAMI KOPO ISIYOKUWA NA RIBA KWA VIJANA
Imewekwa: August 28th, 2025
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Frola Msilu ambae pia ni Mkuu wa idara ya Maendeleo ya Jamii leo amekabidhi pikipiki kumi kwa vikundi viwili vya vijana kutoka Kata za Nkoarisambu na Makiba, ikiwa ni sehemu ya mpango wa mikopo isiyokuwa na riba kwa ajili ya kuinua uchumi wa vijana.
Vikundi vilivyokabidhiwa pikipiki hizo ni pamoja na Kikundi cha Mfungare Boda Boda ambacho kimepokea pikipiki tano, na Kikundi cha Vijana Boda Boda kutoka Makiba ambacho pia kimepokea pikipiki tano.
Kwa upande wao, vijana waliopokea pikipiki hizo wameishukuru Halmashauri kwa kuwaamini na kuwapatia fursa hiyo muhimu, wakiahidi kuzitumia kwa uzalendo, uadilifu na kuhakikisha wanarejesha mikopo kama walivyoelekezwa.
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji amewapongeza vijana hao kwa kuonesha utayari wa kujitegemea na amewasihi kuhakikisha wanazitumia pikipiki hizo kwa malengo yaliyokusudiwa pamoja na kufanya marejesho ya mkopo kwa wakati ili kuwezesha vijana wengine kunufaika na mpango huo.