JUMLA YA WAGOMBEA 8 KUTOKA VYAMA MBALIMBALI VYA SIASA WATEULIWA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ARUMERU MASHARIKI
Imewekwa: August 28th, 2025
Jumla ya Wagombea 10 wa nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki wamerejesha fomu za uteuzi wa nafasi ya Ubunge kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo, miongoni mwa wagombea hao ni Bw.Joshua Nassari (CCM), Mch.Anael Roiya Nassari (ACT WAZALENDO), Singa Maulidi Kalekwa (TLP), Kiwelu Happiness Fredy (MAKINI), Anthonia Michael Ndossi (DP), Happy John Kidadamule (CCK), Kiungai Goodluck Samson (SAU) na Jackline Everest Kimambo wa (CHAUMMA).
Katika uteuzi jumla ya wagombea 8 kutoka vyama mbalimbali wameteuliwa kugombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki.
Akiongea mara baada ya kukabidhi fomu Mch.Anael Roiya Nassari ametoa pongezi kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuwa na utaratibu wa wazi na huru unaoruhusu ushiriki wa vyama vingi bila upendeleo.
Aidha Mgombea wa Ubunge kupitia CCM Joshua Nassari ameahidi kushirikiana na wataalamu pamoja na viongozi wengine kuitetea Arumeru Mashariki endapo atachaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo hili.
Uteuzi wa wagombea wa Ubunge na Udiwani umefanyika siku ya leo tarehe 27.08.2025 kama ilivyo kwa mujibu wa ratiba ya shughuli za Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.