Wananchi wa Halmashauri ya Meru, Wilayani Arumeru wameishukuru Serikali ya awamu ya sita ambapo kupitia kampeni ya siku tatu ya utoaji msada wa kisheria na usuluhishi wa migogoro kwa njia mbadala inayowezeshwa na wizara ya katiba na sheria wameanza kunufaika .
Akizindua kampeni hiyo inayodumu kwa sikuu tatu, Mwl.James Mchembe ambaye ni katibu Tawala Wilaya ya Arumeru akimwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo, amesema serikali ya awamu ya sita imeendelea kuhakikisha wananchi wasio na uwezo wa kumudu gharama za mawakili wanasaidika kwa mujibu wa sheria ya utoaji msaada wa kisheria ya mwaka 2017 ambapo amewataka wananchi kujitokeza katika kampeni inayoendelea katika Kata ya Ngarenanyuki ya utoaji msaada wa kisheria.
Mwl.Mchembe amewataka wataalumu katika kampeni hiyo kuwahudumia wananchi kwa weledi ili kampeni kuwa na tija "wasikilizeni wananchi ili muelewe changamoto zao na kuwasaidia" amehimiza Mwl.Mchembe
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya amesema kampeni hiyo ni fursa kwa wananchi kupata uelewa na msaada wa kisheria sambamba na kujua taratibu mbalimbali "katika kampeni hii mbali na uwepo wa mabanda ya msaada wa kisheria pia uelewa na elimu ya masula mbalimbali inatolewa mfano tuna banda la Maendeleo ya Jamii linaelimisha juu ya taratibu za kupata mkopo usio na riba unaotolewa na Halmashuri"amefafanua Makwinya
Naye Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Meru,ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Ngarenanyuki Mhe.Aminiel Mungure kwa niaba ya wananchi ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusogeza huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi na kuomba Serikali kuendelea kutatua Migogoro ya Ardhi iliyopo ikiwemo ya ngazi za Mikoa na Wilaya.
Laurent Burilo ambaye amemwakilisha Msajili wa mashirika yanayotoa msaada wa kisheria Wizara ya Katiba na Sheria amesema sheria ya utoaji msaada wa huduma za kisheria ya mwaka 2017 inalenga kutimiza azma ya serikali ya kuondoa migogora na kuendeleza amani ambapo ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kupata elimu na huduma bila gharama
Kampeni hiyo ya msaada wa kisheria yenye kauli mbiu " *UTATUZI WA MIGOGORO KWA NJIA MBADALA HUPUNGUZA UADUI NA KUZUIA UMASKINI "* inaendelea katika Viwanja vya Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Ngarenanyuki ambapo wananchi wanahudumiwa na wataalumu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha , Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, wataalum toka Halmashauri wadau toka TLS, LHRC,TAWLA nk,ambapo msaada wa kisheria juu ya masuala ya ardhi ,umiliki wa ardhi,ndoa na mirathi, ukatili wa kijinsia, vizazi na vifo nk unatolewa.
Baadhi ya picha za tukio
Katibu Tawala Wilaya ya Arumeru Mwl.James Mchembe
Diwani Kata ya Ngarenanyuki Mhe.Aminiel Mungure
Mwl.Zainabu Makwinya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Arusha Blandina Nkini
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa