Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI inayoongozwa na Mwenyekiti Mhe. Justine Nyamoga ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa kutekeleza Programu ya Kupanga, Kupima na kumilikisha Ardhi katika Halmashauri yao.
Kamati imetoa pongenzi hizo katika Kikao cha Kamati cha kupokea Taarifa ya Urejeshaji wa Mikopo ya Kupanga, Kupima na kumilikisha Ardhi (KKK) unaotekelezwa katika Halmashauri mbalimbali Nchini kwa Fedha zilizotolewa na Wizara ya Ardhi, kilichofanyika katika Ukumbi wa Anna Makinda Bungeni Jijini Dodoma.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru ilipokea kiasi cha Shilingi 1,655,000,000.00 Fedha hizo zilipangwa kutekeleza mradi wa kupanga, kupima na kumilikisha ardhikatika Shamba la Valeska kwenye Kata za Maroroni na Makiba huku likiwa na ukubwa wa ekari 4087.
Kati Halmashauri ambazo pia zimeweza kurejesha Mkopo wote ni Halmashauri za Wilaya ya Ilemela, Jiji la Mwanza, Wilaya ya Moshi, Morogoro Manispaa, Wilaya ya Mbozi, Wilaya ya Geita, Mji wa Bariadi, Wilaya ya Kilosa, Mji wa Tunduma, Wilaya ya Songwe, Wilaya ya Kaliua, Manspaa ya Kigamboni, Mji wa Kibaha Pamoja na Ofisi ya Ardhi ya Mkoa wa Iringa.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa