• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

MERU DC YAFANYA KIKAO CHA TATHMINI YA LISHE.

Imewekwa: November 8th, 2023

Halmashauri ya Wilaya ya Meru imefanya kikao cha tathmini ya lishe kwa kipindi cha mwezi Julai-Septemba 2023 kwa mwaka wa Fedha 2023/2024.

Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Lishe.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kikão hicho, Mkuu wa Wilayaya Arumeru Mhe. Emmanuela Kaganda ameeleza kuwa suala la Lishe lichukuliwe kwa uzito mkubwa kwani bila kuwa na Taifa lenye Afya bora hatuwezi kuwa na maendeleo.

" Bila kuwa na wananchi wenye afya bora hatuwezi kuwa na maendeleo ya Nchi yetu kwani maendeleo yanatatutwa na watu wenye nguvu na afya" Alisema Kaganda.

Rehema Lema ni Afisa Lishe Halmashauri ya Meru amewasilisha taarifa ya shughuli za Lishe ikiwa ni pamoja na kufuatilia utekelezaji wa mkataba wa Lishengazi ya Kata na Vijiji, Ufuatiliaji wa ukuaji wa watoto chini ya miaka mitano, utoaji wa vidonge(FEFO) vya kuongeza damu kwa wajawazito, Utoaji wa matone ya vitamin A na dawa za Minyoo, unyonyeshaji wa watoto wachanga pamoja na maadhimisho ya siku ya Afya na Lishe Kijiji (SALIKI).

Aidha, Mhe. Kaganda ametoa Maelekezo kwa Afisa Lishe na Watendaji wa Kata zote 26 katika Halmashauri ya Meru kuweka Utaratibu wa kutoa elimu ya Lishe katika maeneo yao.

" Tuongeze wigo wa kutoa elimu ya lishe Makanisani, Msikitini, shuleni na hata kwenye vikao vya kimila ili nao wawe sehemu ya kusambaza elimu lishe kwenye jamii." alisema Mkuu huyo.

Hata hivyo, Mhe. Kaganda ametoa Pongezi kwa Afisa Lishe kwa utoaji wa elimu ya lishe katika Kata ya Ngabobo.

Pia, Pongezi kwa Mkurugenzi Mtendaji Mwl. Zainabu J. Makwinya kwa kuwezesha vikao vya lishe kufanyika.

Vilevile, Mhe. Kaganda amewakumbusha Watendaji wa Kata kutoa elimu kwa wananchi katika maeneo yao kuhusu kutumia mvua hizi zinazoendela kunyesha kupanda mazao ya muda mfupi.

Ikumbukwe kuwa Lishe ni sehemu ya utekelezaji Wa llani ya chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2020 Sura ya 3 Ibara ya 85 ambapo imeelezwa umuhimu wa Lishe "Lishe bora ni muhimu katika kuhakikisha Taifa linakuwa na jamii yenye nguvu kazi imara na uwezo mkubwa wakuelewa na kukabiliana na mazingira yake".


Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • MAADHIMISHO WIKI YA UTYUMISHI WA UMMA 2025 DODOMA

    June 13, 2025
  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa