Halmashauri ya Wilaya ya Meru Leo Tarehe 04.09.2023 imempitisha Mhe. Felister Nanyaro Diwani Viti Maalum Tarafa ya Poli kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Kwa mwaka mwingine wa 2023/2024.
Mhe. Felister Nanyaro amepita bila kupingwa baada ya wajumbe wote waliohudhuria katika Mkutano huo kupiga kura ya ndio.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru ina jumla ya Waheshimiwa Madiwani 35 ambapo wajumbe walioshiriki katika zoezi la kupiga kura walikuwa 32 na wote wamepiga kura ya ndio.
Mhe. Felister Nanyaro ameshika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri kwa kipindi chote cha miaka minne.
Uchaguzi huo ni kwa Mujibu wa Kanuni ya 7 kifungu kidogo cha 3(a) cha kanuni za kudumu za Halmashauri ya Wilaya ya Meru za mwaka 2014, ambapo wajumbe wanatakiwa kumchagua Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri kila baada ya mwaka mmoja wa Serikali.
Aidha, wajumbe wamefanya uchaguzi wa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Halmashauri pamoja na Wenyekiti wa Kamati hizo.
Vilevile, wajumbe wamejadili taarifa ya utendaji na uwajibikaji wa Halmashauri kwa Mwaka uliopita pamoja na kupitisha ratiba ya Vikao vya Halmashauri na Kamati za Halmashauri kwa mwaka 2023/2024.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa