Mhe. Mwanaidi Ally Khamis (Mb) Naibu waziri Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu mapema hii Leo ameendelea na Ziara yake ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru ya ukaguzi na kutambua shughuli zinazo fanywa na shirika la SOS katika kusaidia idara ya Maendeleo ya Jamii ngazi ya Vijiji, Kata Hadi ngazi ya Halmashauri
Aidha kikao alichofanya katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe. Mwanaidi amepokea Taarifa ya utekelezaji ndani ya shirika la SOS inayoeleza juu ya huduma zinazotolewa na kutekelezwa Ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru ikiwemo Malezi mbadala, kupinga Ukatili Kwa Watoto na Wanawake n.k
Kutokana na Taarifa iliyotolewa ya utekelezaji Mhe. Mwanaidi amewataka SOS kuendelea na kazi nzuri wanayoendelea kuifanya aidha kuongeza Nguvu katika upingaji wa Ukatili wa kijinsia hasa Kwa Watoto
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa