fungua hapa kupata video,☝️Wataalam kutoka Shirika la kiserikali na Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania TEMDO wametoa mafunzo ya Matumizi ya Kichomea taka cha kisasa katika Hospitali ya Wilaya ya Meru.
Juma Mzava ni mtaalamu kutoka TEMDO (Tanzania Engineering and Manufacturing Design Organization) ametoa mafunzo ya vitendo ya uendeshaji mtambo na namna unavyotakiwa kufanya kazi ikiwa ni pamoja na kuwasha mtambo, kuweka taka pamoja na hatua nyingine zinazotakiwa kufuatwa.
Pia, ameeleza kuwa mtambo huo ni wa kisasa zaidi na hauna madhara kwa wananchi kwani umezingatia utunzaji wa mazingira na haitoi moshi unaoweza kuleta madhara kwa jamii.
Mtaalamu wa Afya Nicholaus Kataga ameeleza kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kuendesha mtambo huo bila shida na kuweza kufanya kazi kwa kiwango kikubwa zaidi kwani mtambo huo ni wa kisasa kuliko mtambo waliokuwa wakiutumia awali.
Afisa Manunuzi na Msimamizi wa Mradi wa Kichomea taka, Juma Samson ameeleza kuwa Kichomea taka hicho ni kati ya fedha sh. Milioni 900 zilizoletwa za miradi katika hospitali ya Wilaya ambapo kichomea taka hicho imetengewa sh.Milioni 46.
Bw. Samson kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu J. Makwinya ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha za miradi hii na kuhaidi kuendelea kuisimamia ili ikamilike kwa wakati uliopangwa.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa