Katika Kikao kilichofanyika Ukumbi Wa Halmashauri hiyo, Ndg Nyamhokya amesikiliza kero na changamoto za wafanyakazi ikiwa ni njia ya kuyabeba na kuyafikisha ngazi za juu na Serikali ili kutafuta ufumbuzi wa changamoto hizo na kuboresha Maslahi ya wafanyakazi.
Afisa Mwajiri Bw. Raphael Geay amewasilisha ombi Maalum la kufuta Tozo kwa Wastaafu wa Mifuko ya Hifadhi ya jamii.
Mwenyekiti wa TALGWU Wilaya Bw. Said A. Said amewasilisha changamoto ya Watumishi kwenda masomoni kujiendeleza na pindi wanapomaliza masomo na kurejea kazini wanabadilishiwa vyeo ( Recategorization) lakini utaratibu huo unaathiri kupanda kwa Madaraja na inakatisha tamaa.
Pamoja na changamoto zilizojadiliwa katika kikao hicho, kwa niaba ya wafanyakazi wote wa Halmashauri ya Meru, Mwenyekiti wa TALGWU Saidi A. Saidi alitoa Tuzo kwa Ndg Nyamhokya Kwa kutambua mchango wake katika kutetea masilahi ya wafanyakazi na kuhimiza umoja na mshikamano.
Rais wa TUCTA amewahamashisha wafanyakazi ambao hawajajiunga na chama cha wafanyakazi wafanye hivyo.
Katika hatua nyingine, Ndg Nyamhokya na Viongozi wengine wamefanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Meru ofisini kwake kwa lengo la kushauriana namna ambavyo wataweza kusaidia kutetea maslahi ya wafanyakazi.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa