Afisa Elimu wa Elimu ya watu wazima na Elimu Maalumu Mkoa wa Arusha Emmanuel Mahundo alipokuwa kwenye usimamizi shirikishi wa Zoezi la utoaji wa Kinga Tiba ya Minyoo ya Tumbo katika Shule ya Msingi Kilimani.
Aidha Mahundo amewataka Wazazi na walezi wawatoto kuwapeleka watoto wao katika Shule za Msingi zilizo karibu nao ili kuweza kupatiwa Kinga hii Kwa Lengo la kuandaa kizazi Bora na Chenye Afya Bora Kwa Maendeleo yasasa na yajayo. Zoezi hilo linaratibiwa na Dkt. Abdallah Mvungi
Mratibu wa magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele [NTDs] Halmashauri ya Wilaya ya Meru huku Lengo likiwa nikufikia Watoto wenye Umri wa Miaka 5-14
Zoezi hilo limeanza Leo Tarehe 27 na linatarajiwa kuisha Kesho Tarehe 28 Februari 2025 huku likifanyika katika Shule zote za Msingi.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa