• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

UKAGUZI WA MRADI WA UJENZI WA VETA ARUMERU

Imewekwa: December 21st, 2023

Na Annamaria Makweba

Katika Utekelezaji wa Miradi ya ujenzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi 64 vya Wilaya na Kimoja cha Mkoa Songwe , Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknologia imeanza kufanya ukaguzi wa Miradi hiyo ikiwa na lengo la kujiridhisha na utekelezaji wa matumizi ya fedha kwa awamu ya kwanza katika miradi hiyo.

Chuo cha Ufundi Stadi (Veta) kinachojengwa katika Kijiji cha Kisimiri Kata ya Uwiro Wilayani Arumeru ni miongoni mwa Vyuo vinavyojengwa na Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambapo Naibu Waziri Elimu Mhe. Omari Kipanga amefika na kukagua ujenzi wa awali katika chuo hicho.

Katika Maelezo yake Naibu Waziri ameeleza kuwa Wizara ya Elimu inafanya ufuatiliaji wa karibu wa matumizi ya fedha na ubora wa kazi katika miradi yote inayotekelezwa, lengo ni kujiridhisha kazi iliyofanyika lakini pia kuruhusu fedha za awamu ya pili kuletwa na Mradi kuendelea kutekelezwa.

" Wizara inafuatilia miradi hii ili kuona kama ujenzi unaendana na vipimo au michoro iliyotolewa imefuatwa naweza kusema tunaangalia (Value for money) lakini tunaangalia ubora wa kazi" Alisema Kipanga.

Hata hivyo, Mkuu wa Chuo cha Ualimu Elimu Maalum Patandi Lucian E. Segesela ameeleza kuwa Mradi umefikia asilimia 90 ya ujenzi wa majengo yanayojengwa ambayo ni Jengo la Utawala, Majengo 3 ya Karakana, jengo la nyumba ya Mkuu wa Chuo, Jengo la madarasa, jengo la choo, jengo la kibanda cha Mlinzi na Jengo la kupokelea umeme.

Vilevile Diwani Kata ya Uwiro Mhe. Dauson A. Urio ameishukuru Serikali kwa kuleta miradi hii katika Wilaya kwani itasaidia kuboresha mazingira na kuongeza fursa kwa Vijana kujiendeleza na baadae kujiajiri.

Katika hatua nyingine katika Ukaguzi wa Mradi huo, Mhe. Kipanga ametoa maelekezo kwa Meneja wa TANESCO , TARURA na RUWASA Wilaya ya Arumeru kuhakikisha huduma ya Umeme, Barabara na Maji zinapatikana katika maeneo ya mradi ili kurahisisha utekelezaji wa mradi huo.

Ikumbukwe kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imetoa shilingi Bilioni 1.6 ikiwa ni awamu ya kwanza ya utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Chuo hicho.






Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • TAHAPAO NA MERU DC WAWEKA NGUVU KWENYE KAMATI ZA MTAKUWA

    February 19, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa