• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

TICD YAFANYA MATEMBEZI KUHAMASISHA CHANJO UVIKO-19

Imewekwa: December 7th, 2021

Katibu tawala Wilaya ya Arumeru Mwl.James Mchembe ameipongeza Taasisi ya maendeleo ya Jamii Tengeru (TICD) kwa Kushirikiana na Idara ya Afya Halmashauri ya Wilaya ya Meru kufanya matembezi ya hisani ya  kuhamasisha jamii kujikinga na maambukizi ya Uviko-19 ambayo yameambatana  na  utoaji wa chanjo ya UVIKO-19 ,Elimu juu ya magonjwa yasioambukiza na uchangiaji damu.

Akizungumza na hadhara ya Wananchi eneo la Hospital ya Wilaya ya Meru,Mwl. Mchembe ametoa wito kwa wadau wengine kuungana na Serikali kwenye mapambano  dhidi ya UVIKO-19 kwa  kuhamasisha jamii kupata chanjo"Serikali imehakikisha chanjo ya UVIKO-19 inapatikana, nitoe wito kwa Wananchi kupata Chanjo .


Vilevile Mwl Mchembe ametoa rai kwa vijana kuwa mstari wa mbele kupata chanjo hiyo sambamba na kuwa mabalozi wa kuisemea  vyema chanjo hiyo.Pia ametoa wito kwa wadau wengine kuiga taasisi ya TICD.


Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Meru Dkt Maneno Focus amesema Halmashauri hiyo imehakikisha inawafikia Wananchi kwenye maeneo yao kwa kuendesha zoezi la chanjo nyumba kwa nyumba,taasisi za Elimu na dini.Ambapo dozi 4560 Sawa na  asilimila 76 % ya Chanjo zilizopokelewa awamu ya pili zimetolewa kama dozi ya kwanza  na utoaji wa dozi ya pili unaendelea.


Aidha Dkt.Focus ametoa wito kwa jamii kupata Chanjo ya UVIKO-19 ambapo ameainisha kuwa chanjo aina  ya Pfizer imepokelewa na itapatikana katika vituo vyote vya kutolewa huduma.


Naye ,Mkuu wa TICD Tengeru Dkt.Bakari Juma amesema katika kuadhimisha wiki ya maendeleo ya Jamii wamefanya matembezi ya hisani kuunga mkono Juhudi za Mhe.Rais katika mapambano dhidi ya Uviko-19.


Mhe.Juliasi Mungure ambaye ni Diwani wa Kata ya Akheri ametoa wito kwa Wananchi kupata Chanjo kwani  Serikali imeendelea kuhakikisha wanakuwa  salama kwa kuleta chanjo hiyo.

Mwl.James Mchembe akizungumza baada ya  matembezi ya hisani kuhamasisha chanjo ya UVIKO-19 

Dkt.Bakari George akizungumza baada ya  matembezi ya hisani kuhamasisha chanjo ya UVIKO-19 

Mhe.Julias Mungure akizungumza baada ya  matembezi ya hisani kuhamasisha chanjo ya UVIKO-19

Dkt.Maneno Focus akizungumza baada ya  matembezi ya hisani kuhamasisha chanjo ya UVIKO-19 

Picha ya pamoja Meza Kuu na Wanafunzi wa TICD









Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • TAHAPAO NA MERU DC WAWEKA NGUVU KWENYE KAMATI ZA MTAKUWA

    February 19, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa