Wananchi wa Kata ya Seela/ Sing'isi wameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta Fedha nyingi za ujenzi wa Mradi wa Shule mpya ya Sekondari Katika Kata hiyo.
Wananchi hao wametoa pongezi hizo wakati wakishiriki kuchimba Msingi wa ujenzi wa Shule hiyo mpya, ambapo ujenzi huo unafanyika katika eneo la Madira na vijiji vitatu vya Seela, Malala na Sing'isi wameshiriki katika kazi na kuchimba msingi .
Aidha, Viongozi Mbalimbali wa Serikali wameshiriki katika zoezi hilo la awali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Kaganda, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Meru Mwl. Zainabu Makwinya na Diwani wa Kata ya Seela/Sing'isi Mhe. Elisa Nassari ambao wamekuwa mstari wa Mbele kuhakikisha kazi hiyo inaenda vizuri.
Hata hivyo, Askari wa Jeshi la akiba Halmashauri ya Wilaya ya Meru nao wameshiriki katika kuchimba Msingi kama sehemu ya majukumu yao.
Katika hatua nyingine, wananchi wamejitokeza kumpongeza na kuishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Fedha nyingi alizozielekeza katika kata yao fedha za SEQUIP Shilingi Milioni 584,280,028.00 kwani Ukamilishwaji wa Shule hiyo unaenda kukomboa Maelfu ya wanafunzi waliokuwa wanatoka katika Kata hiyo na kwenda Kata nyingine kutafuta elimu ya Sekondari.
Kazi Iendelee
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa