TAARIFA FUPI IDARA YA MIFUGO NA UVUVI.
1.0 UTANGULIZI
1.1 Vitengo
Idara ya mifugo na uvuvi ni moja kati ya idara zilizopo katika Halmashauri ya wilaya ya Meru. Idara ina vitengo vikuu 2 yaani kitengo cha Mifugo na cha Uvuvi. Vitengo vimegawanyika kwenye vitengo 9 vya utendaji kazi. Vitengo hivyo ni:
i. Udhibiti wa magonjwa ya mifugo (Animal Health and Diseases Control)
ii. Uendelelezaji wa Sekta ya Maziwa (Dairy Improvement )
iii. Uendelezaji wa Wanyama Wadogo (Small Ruminant )
iv. Uendelelezaji wa Masoko ya mifugo (livestock marketing)
v. Uendelezaji wa Kuku na ndege wafugwao ( poultry development)
vi. Uendelelezaji wa Malisho (Pasture Development)
vii. Uendelezaji zao la Ngozi (Hides & Skins Development)
viii. Ugani na Takwimu za mifugo (Livestock Extension and Statistics)
ix. Uendelezaji wa Samaki (Fisheries Development)
1.2 Hali ya Ufugaji, Idadi ya wafugaji na mifugo
Asilimia 60% ya wakazi wa Meru ni wafugaji. Kuna jumla ya wafugaji 80,443 wa mifugo mbalimbali na wafugaji157 wa samaki. Mfumo wa ufugaji unaotumika ni ufugaji wa ndani kwa wanaoishi wa ukanda wa juu na kati na ufugaji huria kwa walioko ukanda wa chini. Makadirio ya idadi ya mifugo kwa mwaka 2011 ni kama ifuatavyo: ng’ombe wa asili 151,878, ng'ombe wa maziwa 83,346, mbuzi wa asili 170,263, mbuzi wa maziwa7,601, kondoo126,990, nguruwe 3,220, kuku wa asili 273,709, kuku wa kisasa 220,152, mbwa 8,998, paka 6,030, bata 6258, ngamia 37, punda 16,352 sungura 3,266, bata mzinga 183, kanga 114, bata bukini 121 na farasi 14.
1.3 Miundo mbinu
Meru ina majosho 22 ambapo majosho 4 tu ndio yanafanya kazi nayo ni josho la Olkunqw’ado, Nnkuuny – Uwiro, LITA -Tengeru na NAIC –Usa river. Majosho mengine 18 ni mabovu na yanahitaji ukarabati na mengine yanabidi yahamishwe kutokana na sababu mbalimbali. Majosho mabovu ni josho la Manyata Lekitatu, Maweni, Majengo, Mbuguni, King’ori, Leguruki, Mikuuni, Uzunguni, Belemu, Karangai, Maji ya chai, Ngabobo, Kalasia, Kikatiti, Maroroni, Nambala, Mwakeni na Kisimiri juu. Miundo mingine na idadi ni Malambo 3, Birika za kunywea maji 21, Vituo vya Afya ya Mifugo 2, Machinjio 2, Karo za kuchinjia 37, Vibanio 4, Mabanda ya ngozi 3, Vituo vya kuzalisha vifaranga vya kuku 3, maduka ya pembejeo za mifugo 47, minada ya mifugo 3 na mabwawa ya samaki 471.
2.0 NGUVUKAZI YA IDARA YA MIFUGO NA UVUVI
Idara ya Mifugo na Uvuvi ina jumla ya watumishi 52 wanaume 42 wanawake 10 Watumishi 50 ni wa fani za Mifugo na watumishi 2 ni wa fani za Uvuvi. Watumishi 10 wako Makao Makuu, katika ngazi ya Kata wako 22 na Vijiji 17 na watumishi 3 wapo masomoni katika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine .
2.1 Vitendea kazi
Idara ina pikipiki 10, Komputa za mezani 2, Komputa mpakato 1, printer 1, jokofu 2 moja mbovu, mitungi ya uhimilishaji 20, Veterinary kits 3, Cool boxes 3, Kabati 2 na Bunduki 1.
KITENGO CHA UGANI WA MIFUGO
Kitengo hiki kinashughulika na utoaji wa huduma za ugani wa mifugo kwa wafugaji kwenye kata na vijiji kwa kutumia Maafisa Ugani wa Mifugo. Aidha, Wataalamu wa mifugo na Samaki ngazi ya wilaya pia hutoa huduma za Ugani wa mifugo na samaki wenye kata na vijiji penye uhitaji na shughuli maalumu zinapojitokeza.
Idadi ya Maafisa Ugani wa Kata na Vijiji
Halmashauri ya Meru ina maafisa Ugani wa mifugo 39. Kuna Maafisa Ugani Mifugo wa Kata 22 kwenye kata za Nkoanrua, Ambureni, Nkoarisambu, Akheri, Seela Sing’isi, Poli, Nkoaranga, Nkoanenkoli, Songoro, Usa-River, Maji ya Chai, Imbaseni, Kikatiti, King’ori, Malula, Maruvango, Leguruki, Ngarenanyuki, Ngabobo, Maroroni, Kikwe na Shambarai Burka. Kata 4 ambazo hazina Maafisa Mifugo wa Kata hizo ni Makiba, Majengo, Uwiro na Mbuguni. Hata hivyo jitihada zimefanyika za kuhakikisha hazikosi huduma kwani kuna Maafisa Mifugo wa Kata wa kata zingine wanakaimu nafasi hizo mpaka watakapopatikana. Kuna Maafisa Mifugo wa Vijiji 16 Kipande Nkoavele, Ambureni, Akheri, Patandi, Seela, Ndatu, Ngyani, Sangananu, Urisho, Mulala, Manyata, Lekitatu, Ngurdoto, Kitefu, Ngyeku, Nambala. Vijiji 76 havina wataalamu lakini vinahudumiwa na maafisa mifugo wa kata. Kuna mratibu 1 wa huduma ya uhimilishaji wa Wilaya ambae kituo chake cha kazi ni kata ya Poli.
Shughuli kubwa ni:
· Kushiriki kwenye kupanga na kutekeleza mipango mbali mbali ya maendeleo ya mifugo na uvuvi
· Ushauri kwenye ufugaji
· Tiba kwenye mifugo
· Ukaguzi wa nyama
· Mafunzo kwa wakulima wafugaji
· Kuratibu vikundi vya wafugaji katika masuala ya ufugaji
· Kuwezesha upatikanaji na utumiaji wa teknolojia na taarifa mbalimbali za mifugo kwa wafugaji
· Daraja kati ya watafiti na wafugaji kwenye mikutano, majaribio n.k yanayohusiana na teknolojia za mifugo
· Kushirikana na sekta binafsi katika masuala ya kuendeleza mifugo na uvuvi
Changamoto kubwa ni:
· Upungufu wa watumishi 4 wa ngazi ya kata na upungufu mkubwa wa watumishi 76 wa ngazi ya kijiji
· Uhaba wa Vitendea kazi hasa vya tiba kwa mifugo
· Uhaba wa vyombo vya uhakika vya usafiri hasa pikipiki
· Maeneo makubwa ya Kutoa huduma kulingana na idadi ndogo ya wataalamu
· Ukosefu na ubovu wa Miundo mbinu ya mifugo iliyopo mfano majosho, minada
MAELEZO MAFUPI YA KITENGO CHA KUDHIBITI MAGONJWA YA MIFUGO.
Magonjwa ya mifugo ni kati ya matatizo yanayokabili maendeleo ya tasnia ya mifugo. Katika Halmashauri ya Meru yapo baadhi ya magonjwa yenye athari kiuchumi katika uzalishaji wa mifugo ambayo ni pamoja na magonjwa ya kiwele, Chambavu, Ndigana Kali, Ndigana baridi, Maji moyo, Mkojo Mwekundu, Homa ya mapafu, Ugonjwa wa kwato na midomo, Minyoo, pamoja na magonjwa ya ngozi, uzazi na yale yanayosababishwa na ukosefu wa virutubisho,
Kwa upande wa kuku magonjwa muhimu ni pamoja na Marek’s, Homa ya matumbo, Mycoplasma, Ndui ya kuku, Gumboro, Koksidia, Mafua ya kuku, Kipindupindu cha kuku, Utitiri, na Chawa.
Aidha yapo magonjwa yanayoibuka ambayo yana athari kubwa kiuchumi na kwa
afya ya binadamu. Magonjwa muhimu ya mifugo yanayoambukiza binadamu ni Kichaa cha Mbwa, Ugonjwa wa Kutupa Mimba, Kifua Kikuu, Kimeta, Malale, Tegu wa Nguruwe na
Ng’ombe na Salmonellosis. Hivyo kitengo cha kudhibiti magonjwa ya mifugo kimeimarisha utoaji wa huduma za kitaalam katika kudhibiti magonjwa ya mifugo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama vile Mbwa wa Afrika, Meru animal welfare organization (MAWO), Hifadhi ya Taifa ya Arusha (ANAPA).
1. SHUGHULI ZINAZOFANYIKA;
1. Kutoa huduma za afya ya mifugo.(kutoa tiba, kuhasi, kukata kwato, uhimilishaji,kukata meno, kukata midomo, kukata mikia)
2. Kuratibu na kusimamia shughuli za usafi wa machinjio na ukaguzi wa nyama.
3. Kutoa chanjo na matibabu kwa mifugo aina mbalimbali.
4. Kushiriki katika uchunguzi wa magonjwa ya mifugo.
5. Kusimamia na kuratibu uzingatiaji wa Kanuni na Sheria za Magonjwa, ukaguzi wa mifugo na mazao yake na pembejeo za mifugo.
6. Kusimamia haki za wanyama.
7. Kutayarisha na kusimamia mipango ya kuzuia, kudhibiti na kutokomeza magonjwa ya mifugo.
8. Kuandaa taarifa za afya ya mifugo.
Chanjo ya kichaa cha mbwa.
Uchunguzi wa magonjwa ya mifugo
Hereni kwa ajili ya utambuzi wa mifugo
TAARIFA FUPI YA KITENGO CHA MAZIWA IDARA YA MIFUGO NA UVUVI.
1. UTANGULIZI
Ni kitengo kinacho jihusisha na kuendeleza sekta ya maziwa wilayani ikiwa ni pamoja na uzalishaji, usindikaji na masoko ya maziwa na bidhaa zake.
2. Shughuli mbalimbali zilizofanyika na zinazoendelea kwenye kitengo
Ø Mafunzo.
Kutoa mafunzo mbalimbali kama ufugaji bora wa wa maziwa, usindikaji wa maziwa, ujasiria mali katika ng’ombe wa maziwa. Mafuzo hutolewa na maafisa ugagani waliopo kwenye kata na vijiji kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Ø Uratibu wa vikundi vya uzalishaji na usindikaji wa maziwa.
Halmashauri ina jumla ya vikundi 14 vya usindikaji na ukusanyaji wa maziwa. Vikundi hivyo ni Medafa, Agape, Uvingo, Inuka, Jitume, Llima-numbe, Medawofa, ukombozi, Ngyni Speciality, Manna, Nkole, Kyuta, Mountain Green, na Pendaneni.
Ø Tunapanga na kutekeleza miradi mbalimbali ya ngombe wa maziwa.
Mfano DADPs, Public Private Partnership for Artificial Inseminatition Delivery (PAID) na African Dairy Genetic Gain (ADGG).
Ø Kusimamia sheria ya maziwa katika katika Wilaya.
Ø Kushirkiana na kuratibu wadau katika mikutano, makongamano, Warsha, maonesho mbalimbali yanayohusiana na ufugaji, usindikaji, biashara ya maziwa na bidhaa zake mfano wiki ya maziwa kitaifa na maonesho ya Kilimo nanenane. Mfano MIVARF imefadhili wiki ya maziwa Kitaifa mwaka huu ambayo yalifanyikia Bukoba ambapo wataalamu wawili wa Idara ya Mifugo na Uvuvi walihudhuria, wasindikaji wanne kutoka viwanda vilivyopo kwenye Halmashauri ya Meru navyo ni Mountain Green na Grand Demam, mwakilishi kutoka MIVARF na mwakilishi wa wadau wa Sekta ya Maziwa Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Ø Uendelezaji wa Sekta ya maziwa
Miradi mbalimbali imetekelezwa kwa kushirikiana na wadu wa maendeleo ili kuendelza sekta ya maziwa mfano mradi wa kujenga chumba cha kupoozea maziwa (cold room) kwenye kiwanda cha Grand Demam kilichopo USA River, ambao una gharimu jumla ya shilingi 27,250,000/= mradi ambao unafadhiliwa MIVARF kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Ujenzi wa Kiwanda cha Llmanumbe na ununuzi wa power Tiller kwaajili ya kukusanyia maziwa kwa kikundi cha Medafa miradi hii ilifadhiliwa na District Agriculture Development plans (DADPs)
Kiwanda cha Grand Demam
|
|
|
|
Kituo cha kukusanyia maziwa cha MEDAFA
MFUGAJI WA NG’OMBE WA MAZIWA AKIKAMUA MAZIWA
GARI LA KUBEBEA MAZIWA NA BIDHAA ZAKE
MFUGAJI AKIPELEKA MAZIWA KWENYE KITUO
GARI MEDAFA LIKIPELEKA BIDHA ZA ZAO LA MAZIWA SOKONI
POWER TILER LIKIPELEKA MAZIWA KIWANDANI MEDAFA
TANKI LA KUPOOZEA MAZIWA LA KIWANDA CHA MEDAFA
AFISA UGANI AKIENDA KUFANYA UHIMILISHAJI
KITENGO CHA NGOZI
Kitengo hiki kinahusika na kuhakikisha kunakuwa na uzalishaji, utayarishaji usindikaji, uchakatajiwa na utengenezaji wa ngozi na bidhaa zake. Ngozi hizi ni za wanyama wafugwao kama ng’ombe, mbuzi na kondoo.
Shughuli zinazofanyika:
· Kutoa Mafunzo kwa wadau wa ngozi juu ya ufugaji bora, uchunaji, ukusanyaji na uwekaji madaraja ya ngozi na uongezaji thamani ya ngozi
· Ushauri wa uboreshaji zao la ngozi
· Kusimamizi na utekelezaji wa sheria mpya ya biashara ya ngozi Na. 18 ya mwaka 2008 pamoja na marekebisho ya mwaka 2014
· Ukarabati/ujenzi wa Miundombinu ya ngozi sehemu ya kutengeneza na kuhifadhi ngozi kama machinjio na mabanda ya ngozi. Mfano tumekarabati machinjio ya Tengeru na kujenga banda la ngozi la Kikatiti
· Kuhamasisha uundaji wa vikundi vya ngozi na Kuimarisha vilivyopo
· Kushawishi na kushirikiana na sekta binafsi kuanzisha biashara/miradi/viwanda vya kutengeneza bidhaa za ngozi
· Kuwezesha upatikanaji wa habari na kutuma kwa wadau
· Usimamizi, ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa shughjuli za mradi wa ngozi
KITENGO CHA UENDELEZAJI WA SAMAKI
Majukumu makubwa ya kitengo hiki ni kusimamia shughuli mbalimbali za ukuzaji wa viumbe kwenye mabwawa (Aquaculture) pamoja na kusimamia rasilimali za uvuvi katika ziwa Duluti ikiwa ni pamoja na doria za mara kwa mara kudhibiti uvuvi haramu katika ziwa hilo.Aina ya samaki wanaofugwa kwa kiasi kikubwa ni Sato (Oreochromis niloticus),na Kambale (Clariusspp).
Majukumu mengine ni Kudhibiti usafirishaji wa samaki na mazao yake usiofuata sheria na taratibu.Shughuli za kitengo zinaongozwa na sera ya taifa ya uvuvi ya mwaka 2015, sheria ya uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 pamoja na kanuni ya uvuvi ya mwaka 2009.
Fursa zilizopo
i. Uwepo wa wataalamu wa ukuzaji wa viumbe vya majini katika kitengo cha uvuvi
ii. Uwepo wa taasisi binafsi na za serikali zinazojihusisha na miradi ya utoaji wa Elimu ya ufugaji wa samaki ni fursa ya yakujifunza kwa vitendo (LITA Tengeru na World Vision)
iii. Uwepowa maji safi ya kutosha kwenye maeneo mengi yenye ubora kwa ajili ya kufugia samaki.
iv. Mwamko mkubwa wa wananchi juu ya ufugaji wa samaki nifursa kwa ajili ya uwekezaji kwenye uzalishaji wa vyakula pamoja na vifaranga wa samaki.Mpaka sasa kuna wafugaji wanaokadiriwa kufikia 157 pamoja na mabwawa yanayokadiriwa kufikia 471
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa