UZINDUZI WA JENGO LA TEHAMA SHULE YA SEKONDARI PATANDI MAALUM
Imewekwa: August 15th, 2025
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe. Mwinyi Ahmed Mwinyi mapema hii leo ameshiriki uzinduzi wa jengo la kiteknolojia lenye miundombinu ya intaneti na kompyuta mpakato pamoja na kupokea changamoto mbalimbali zinazo ikumba shule hiyo.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Arumeru ambae pia amekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ameahidi kutoa ushirikiano wakutosha katika kuhakikisha anatoa msaada wa hali na Mali ili kuweza kusaidia shule hiyo ambayo inatoa elimu kwa vijana wenye mahitaji maalumu.
Pia ametoa Shukrani za dhati kwa mzamini mkuu wa msaada huo FSE ambao wamewezesha upatikanaji wa Jengo hilo na Vifaa vyote vya muhimu vya utendaji kazi ambao utakwenda kurahisiha zoezi la ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi na walimu katika shule hiyo. Mwisho ametoa Shukrani za dhati kwa walimu ambao wanafanya kazi ya kiungu yakutoa huduma kwa vijana waliopo katika shule hiyo.