Halamshauri ya Meru imetenga eneo la ekari 25 kwa ajili ya kujenga kituo cha kisasa cha malori makubwa kwa ajili ya kupakia na kushusha mizigo.
Eneo hili litakuwa na miundombinu kama vile Garage, Car wash, Fence na Maghala (Warehouses) kwa ajili ya kuhifadhia mizigo. Mradi utakuwa na mitambo ya kisasa ya kupakia na kushusha mizigo.
Lengo la mradi huu ni kupunguza msongamano unaosababishwa na malori makubwa ya mizigo yanayoingia katikati ya Jiji la Arusha.
Mradi utakapokamilika, malori makubwa ya mizigo hayataruhusiwa tena kuingia katikati ya Jiji. Mizigo itakuwa ikishushwa katika kituo hiki na malori chini ya Tani 10 ndio yatakayoruhusiwa kuingia katikati ya Jiji.
Miundombinu ya maji, umeme iko jirani lakini pia eneo hili liko pembeni ya barabara ya lami (Arusha-Moshi).
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa