Imetolewa na ofisi ya Habari Mkoa wa Arusha.tovuti (www.arusha.go.tz).
Mwenge wa uhuru utawasili katika mkoa wa Arusha tarehe 12 Septemba 2018 ukitokea mkoani Mara.
Utapokelewa Olduvai Gorge kata ya Ngoile wilayani Ngorongoro.
Ukiwa katika mkoani wa Arusha utakimbizwa katika Halmashauri zote 7 za mkoa.
Mwenge utaanzia kukimbizwa katika wilaya ya Ngorongoro,Karatu,Monduli, Longido,Arumeru na kumalizia Jiji la Arusha.
Mwenge ukiwa katika mkoa wa Arusha utakimbizwa umbali wa kilometa 1,114.9.
Utakagua,kuzindua,kufungua na kuweka jiwe la msingi miradi ipatayo 46 yenye thamani ya kiasi cha shilingi za tz 36,182,058,694.35 .
Ambapo mchango wa serikali Kuu ni Tsh 7,416,735,688.35, mchango wa wahisani mbalimbali ni Tsh 13,247,332,956, kutoka halmashauri michango ni Tsh 479,529,350 na michango ya wananchi ni Tsh 15,038,460,700.
Mwenge utaweka jiwe la msingi miradi 9,4 itafunguliwa,22 itazinduliwa na 11 itakaguliwa katika halmashuri zote.
Mwenge utamalizia kukimbizwa katika wilaya ya Arusha na kukabidhiwa mkoani Manyara Septemba 19,2018 katika wilaya ya Babati.
IKUMBUKWE
Mwenge wa Uhuru utakimbizwa tarehe 17 Septemba 2018 katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa