DIB YATANGAZA NEEMA KWA WANANCHI MUFILISI WA BENKI YA WANANCHI MERU ( MERU COMMUNITY BANK).
Imewekwa: March 29th, 2024
Bodi ya Bima ya Amana (Deposit Insurance Board) DIP imetoa mafunzo ya bima ya amana na ufilisi kwa Watendaji wa Vijiji, Wataalam na Wadau mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Meneja uendeshaji wa bodi ya bima ya Amana Nkanwa Magina amesema kuwa bodi hiyo imeamua kuendesha mafunzo hayo Ili kuwezesha wananchi kuelewa majukumu ya bodi hiyo ambayo ni kinga ya amana za wateja kwenye benki na taasisi za kibenki ambayo inawasaidia kuweza kupata fedha zao pindi taasisi hizo zinapokuwa mufilisi.
Aidha, Magina amesema kuwa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Meru mafunzo yatatolewa katika Kata ya Akheri eneo la Tengeru, Leganga, Usariver pamoja na Kikatiti kwa lengo la kuwapata wananchi na wafanyabiashara wengi ambao walikuwa na amana zao katika Benki ya Wananchi Meru au "Meru Community Bank".
Mafunzo hayo yametolewa na Mkuu wa Idara ya Utawala Joyce Shala na Mhasibu Mwandamizi Silvani Makole kutoka DIB. ambapo kwa nyakati tofauti wametoa ufafanuzi kuhusu mamlaka ya bima za amana, malengo ya mfumo wa bodi ya amana, amana ambazo hazifidiwi na bima ya amana, ulipaji wa mikopo, uuzaji wa mali za benki.
Aidha, Meneja huyo amewataka Watendaji wa Vijiji kufikisha elimu hiyo kwa wale wote ambao waliokuwa na Amana katika benki iliyokuwa ya Wananchi Meru kwenda kuchukua amana zao katika Benki ya Posta (TPB).
Bodi hiyo mbali na kutoa elimu hiyo kwa wananchi wa Meru lakini ina mikakati ya kuendelea kutoa elimu kwa maeneo mengine ambayo baadhi ya benki zao zilikuwa mufilisi ili kuwawezesha kutambua kuwa taasisi za kifedha au benki zinazofungwa akiba zao bado zitakuwepo.