Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Ndg. Thomas Ole Sabaya amesifia utendaji Kazi wa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Kaganda katika kikao kilichowakutanisha Watumishi wa Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru na Wajumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Arusha wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo kama sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya Mwaka 2020.
Ndg. Sabaya amesema kuwa amefurahishwa kwa DC Kaganda kuendelea kuaminiwa na kubaki Arumeru kuendelea kuwatumikia wananchi.
"Kwa kazi unayofanya tumefurahi sana wewe kubaki hapa Arumeru. Lakini pia tumefurahi na Mkuu wetu wa Mkoa wa Arusha kubaki hapa" amesema Sabaya.
Aidha, ameeleza kuwa Mkuu wa Wilaya Kaganda amefanya mambo makubwa kabla ya kuja hapa na baada ya kuja hapa kazi zake ni nzuri na zinaonekana