Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru anawatangazia wananchi wote kuwa kutakuwa na mkutano wa baraza la Halmashauri hiyo utakaofanyika tarehe 08 na 09 Novemba 2018 kuanzia saa 4:00 kamili asubuhi.
Mkutano huo ni wa kawaida kwa mujibu wa sheria za Serikali za mitaa, utajadili shughuli za maendeleo kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai hadi Septemba kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Mikutano huo utafanyika katika ukumbi wa Halmashauri .
Wananchi wote wa Halmashauri ya Meru mnakaribishwa.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa