Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Will J. Njau wakati wa ufunguzi wa mkutano wa robo ya 3 wa baraza la Halmashauri hiyo amesema mbali na changamoto ndogo ndogo zilizopo kwenye Halmashauri hiyo ,Mwenendo wake unaridhisha kwani ukusanyaji wa mapato umefikia asilimia 71.88 kiasi ambacho ni cha juu ikizingatia kuna vyanzo kama 3 vilivyotwaliwa na Serikali kuu kikiwemo ushuru wa mabango, pia Halmashauri hiyo imezawadiwa gari kwa kufanya vizuri kwenye Usafi na Mazingira , pia imeshika nafasi nzuri kwenye ufaulu wa shule za sekondari na msingi .
Baadhi ya wajumbe ambao ni madiwani wamelalamikia kitendo cha fedha za miradi ya maendeleo kutokupelekwa jambo linalosababisha miradi mingi kusimama kwenye Kata ambapo makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,Nelson Mafie ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya fedha ,mipango na utawala amewashauri wajumbe hao kujiridhisha kama miradi wanayoisemea ipo kwenye bajeti.
Nae Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Dkt.Amani Sanga amefafanua kuwa kwa mwaka wa fedha 2017/2018 Halmashauri hiyo ilipitisha kwenye bajeti yake fedha kutoka mapato yake ya ndani kiasi cha Biliono 2,226,374,000 kwa ajili ya miradi ya maendeleo hadi sasa zaidi ya milioni 350,270,430 ya fedha hizo imepelekwa kwenye miradi ya maendeleo ,pia amesema fedha zinazopelekwa kwenye miradi ya maendeleo hutegemea ukusanyaji wa mapato.
Aidha mkutano huo wa baraza la Halmashauri ya Wilaya ya Meru ambao ni wa siku 2 umehairishwa kwa siku ya kwanza ukiwa na azimio kuwa halitapokea taarifa za utekelezaji wa kata ambazohazija fuata utaratibu wa kisheria wa kujadiliwa na kupitishwa kwenye baraza la maendeleo ya Kata (WDC) .
PICHA ZA TUKIO.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru akizungumza wakati wa mkutano wa baraza lka Halmashauri hiyo kwa kipindi cha lrobo ya 3,kushoto kwake ni makamu wa Halmashauri hiyo mhe.Diwani Nellson Mafie na kulia kwake ni Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Amani Sanga.
Baadhi ya waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakiwa kwenye mkutano wa baraza la Halmashauri hiyo kwa kipindi cha robo ya 3.

Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru ,Wakili Makdalena John akitoa ushauri wa kisheria wakati wa mkutano wa baraza la Halmashauri hiyo kwa kipindi cha robo ya 3.
Mkuu wa idara ya Utawala na Rasilimali watu kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru Grace Mbilinyi akitoa ufafanuzi unaohusu masuala ya kiutumishi yaliyohojiwa na wajumbe kwenye mkutano wa baraza la Halmashauri hiyo kwa kipindi cha robo ya 3.
Baadhi wakuu wa idara na vitengo/wawakilishi wa wakuu wa idara na vitengo wakiwa kwenye mkutano wa baraza la Halmashauri hiyo kwa kipindi cha robo ya 3.
Baadhi wakuu wa idara na vitengo wakiwa kwenye mkutano wa baraza la Halmashauri hiyo kwa kipindi cha robo ya 3.
Baadhi wakuu wa idara na vitengo wakiwa kwenye mkutano wa baraza la Halmashauri hiyo kwa kipindi cha robo ya 3.
Baadhi watumishi wa serikali na wananchi wakiwa kwenye mkutano wa baraza la Halmashauri hiyo kwa kipindi cha robo ya 3.
Baadhi wawakilishi wa wakuu wa idara na watumishi wa Serikali wakiwa kwenye mkutano wa baraza la Halmashauri hiyo kwa kipindi cha robo ya 3.
Baadhi wakuu wa vitengo/wawakilishi wa wakuu wa idara wakiwa kwenye mkutano wa baraza la Halmashauri hiyo kwa kipindi cha robo ya 3.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa