Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Mashariki Ndg.Emmanuel J. Mkongo amekabidhi tena, fomu za Uteuzi kugombea Ubunge Jimbo hilo kwa wateule wawili Goodluck Kiungai kupitia Chama cha Sauti ya Umma (SAU) na Ndg.Mohammed Bakari Sauko kupitia chama cha (NRA).
Wagombea wote wawili walifika kwenye Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi kwa nyakati tofauti na kukabidhiwa fomu hizo za Uteuzi kuwania nafasi ya Mbunge wa Jimbo hilo.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo, alimkabidhi fomu ya uteuzi wa nafasi ya Ubunge Goodluck Kiungai kupitia Chama cha SAU mnamo saa 3:49 asubuhi. Pia Mohammed Bakari Sauko kupitia chama cha (NRA) alikabidhiwa fomu hiyo majira ya saa 8:45 mchana.
Aidha Msimamizi huyo wa Uchaguzi, amewakabidhi fomu ya Uteuzi wagombea hao, kufuatia Maelekezo ya Fomu ya Uteuzi Na. 8B, kwa mujibu wa Kifungu cha 38 (3) na (4) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343 ikiweka wazi mambo yaliyojumuishwa kwenye fomu ya Uteuzi.
Wagombea hao wawili wamefanya kufikisha idadi ya waliochukua fomu hizo Jimboni humu kufikia 7 kutoka vyama 7 vya siasa.
Aidha wateule hao 7 waliochukua fomu za uteuzi toka zoezi la utoaji fomu kuanza tarehe 12/08/2020 wanatoka vyama vya DM,ADC,UMD,UPDP,AAFP,SAU ,NRA.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Mashariki Ndg.Emmanuel J. Mkongo (kulia)akikabidhi fomu za uteuzi kwa Goodluck Kiungai kupitia Chama cha Sauti ya Umma (SAU) .
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Mashariki Ndg.Emmanuel J. Mkongo (kulia)akikabidhi fomu za uteuzi kugombea nafasi ya Ubunge kwa Mohammed Bakari Sauko kupitia chama cha (NRA).
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa