Halmashauri ya Meru ina vivutio vingi vya utalii ambavyo vinapatikana ndani ya wilaya vivutio hivyo ni kama vile misitu ya asIli iliyofunga yenye wanyama mbali mbali kama vile mbega weupe,kima,tumbili,dik dik,ndege pamoja na wadudu watambaao kama vile nyoka vivutio vingine ni Maanguko ya maji,mapango makubwa ya kale,makaburi ya wamisheni wa kwanza Tanzania na eneo maarufu kwa mila ya Wameru liitwalo Mringaringa lenye miti mikubwa ya asili ambayo jamii ya wameru iliitumia kufanyia matambiko ya kimila,kivutio kingine ni Milima ambayo shughuli za upandaji(hiking activities) zinaweza fanyika
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa