Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Mashariki anawataarifu Wasimamizi wa vituo na Makarani waongozaji kuhudhuria kwenye semina ya mafunzo ya uchaguzi tarehe 25.10.2025 kwa Makarani Waongozaji na tarehe 26 hadi 27.10.2025 kwa Wasimamizi wa Vituo. Semina itafanyika kwenye Ukumbi wa mikutano wa NGURDOTO LODGE kuanzia saa 01:00 asubuhi. Kila mshiriki anakumbushwa kufika na moja ya kitambulisho mfano Kitambulisho cha Taifa (NIDA), Kitambulisho cha mpiga kura, kitambulisho cha kazi au leseni ya udereva.
Kupata orodha ya majina ya washiriki Bofya hapa: ORODHA_YA_WASIMAMIZI_NA_MAKARANI_WA_VITUO_VYA_KUPIGIA_KURA_WALIOITWA_MAFUNZONI_UCHAGUZI_MKUU_2025.pdf
"Kura yako haki yako Jitokeze kupiga Kura"
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa