Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Damari Mchome ametoa rai kwa jamii katika Halmashauri hiyo kukamilisha miundombinu mbalimbali katika shule za Sekondari walizozianzisha ili taratibu za usajili zifuate na wanafunzi kuweza kunufaika na elimu bila malipo.
Mwl. Mchome amefafanua kuwa Miundombinu inayohitajika ili shule ya Sekondari isajiliwe ni lazima kuwe na madarasa 4 yenye samani yaani meza na kiti nk , maabara 3, ofisi ya Walimu , nyumba za Walimu , vyoo vya Wanafunzi na Walimu
Aidha kwa mujibu wa taratibu shule za sekondari yaani za kata ni za wananchi hivyo wanajukumu la kujenga miundombinu inayohitajika .
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa