Katika uchaguzi huu Mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani Jimbo la Arumeru Mashariki lilikuwa na vituo 521 vya kupiga kura katika Kata 26.Pia idadi ya wapiga kura walioandikishwa jimboni humo ilikua 194 ,367.
Aidha Kata 20 pekee ndio zilizo kuwa na uchaguzi wa Madiwani kwani Kata 6 zilizobakia wagombea wake walipita bila kupingwa wakati wa zoezi la awali la uteuzi wa Wagombea.
Baada ya zoezi la kuhesabu kura kukamilika katika vituo vya kupiga Kura wagombea watokanao na Chama cha Mapindizi (CCM) wameongoza katika kata zote 20 zilizokuwa na uchaguzi wa Madiwani hivyo kupelekea Chama hicho kuongoza katika Kata zote 26.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa