Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru anawatangazia Wananchi wakazi wa Halmashauri hiyo kuhudhuria Mkutano wa kawaida wa Baraza la Halmashauri hiyo (Full Council)k wa robo ya pili mwaka wa fedha 2020/2021, kwa kipindi cha kuanzia Oktoba hadi Desemba 2020. Mkutano huo utakaofanyika kwa Siku mbili, tarehe tarehe 1 -2 Januari 2021, katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo, kuanzia saa 4:00 kamili asubuhi.
Mkutano huo wa baraza la Madiwani utakuwa na ajenda 7, huku agenda kuu zikiwa ni pamoja na kuwasilisha taarifa za utekelezaji za Kata kwa kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2020,Maswali ya papo kwa papo kwa Mwenyekiti na Mkurugenzi,Kuwasilisha taarifa za kudumu za Halmashauri kutoka kwa wenyeviti wa Kamati hizo.
Mkutano huo ni wa kawaida kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za Serikali za Mitaa. Mkutano Baraza la Madiwani ni Mkutano wa wazi, hivyo wananchi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru wanakaribishwa.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa