KUTOKA WILAYANI ARUMERU.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mkoani Arusha imezidi kuangaza nuru ya Elimu bora kwa kushika nafasi ya 18 kitaifa katika ubora wa ufaulu upimaji wa darasa la nne mwaka 2018.
Aidha nafasi hiyo ya 18 kitaifa ni mafanikio makubwa kwa Halmashauri hiyo kwani imesogea nafasi 33 za ufaulu ikiwa ni kutoka nafasi ya 51 kitaifa iliyoshika mwaka 2017 hadi nafasi ya 18 kitaifa iliyoshika mwaka 2018.
Sambamba na kuwa nafasi ya 18 kitaifa katika ubora wa ufaulu wa upimaji darasa la nne, Halmashauri ya Meru imeshika nafasi ya pili kimkoa huku nafasi ya kwanza ikichukuliwa na Halmashauri ya Jiji la Arusha .
Matokeo hayo ya Upimaji wa Kitaifa wa darasa la nne uliofanyika 2018 yametangazwa rasmi mjini Dodoma na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania Dkt Charles Msonde .
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa