Wananchi wa Kata ya Nkoanekoli Halmashauri ya Wilaya ya Meru,Wameshauriwa kupanda miti ya asili aina ya Msesewe, Mruka, Moliondo, Mwarille na Mringaringa ili kuondokana na uharibifu wa mdudu mchwa.
Afisa Maliasili wa Halmashauri hiyo Ndg.Charles Mungure amesema Kata ya Nkoanekoli ni miongoni mwa maeneo yalliyopitiwa na bonde la ufa,hivyo udongo wake unakiwango kikubwa cha chumvichumvi ambacho huwavutia wadudu (Mchwa) kuweka makao.
Aidha Mungure ameeleza kuwa Mti Ulaya (Grevelia ) ambao wananchi hao wamekua wakiupanda unakiwango kikubwa cha Sukari ,ambacho huwavutia wadudu(Mchwa ) kushambulia mizizi ya miti hiyo hadi kupelekea kukauka.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa