Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru anawatangazia wajasiliamali wadogo ambao hawajachukuwa vitambulisho kuwa, Halmashauri ya Meru imehakikisha mjasiliamali anapata kitambulisho bila adha kwa kuvisogeza vitambulisho hivyo kwenye ofisi za Watendaji wa Kata na Vijiji maeneo waliyopo.
Aidha ili kupata kitambulisho Mfanyabishara anatakiwa kufika Ofisi ya Kijiji au Kata akiwa vitu vifuatavyo:-
1.Picha mbili(passport size)
2.Kitambulisho chochote
3.Fedha taslimu shilingi elfu ishirini (20,000/=) kwa ajili ya kitambulisho.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa