Kutoka Wilayani Arumeru.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Bw.Emmanuel Mkongo anawatangazia wananchi wote waliopewa maeneo ya kujenga vibanda kwenye maeneo ya soko la Tengeru ambao mpaka sasa hawajaonesha juhudi zozote za kuendeleza maeneo hayo, kuwa watakuwa wamepoteza sifa ya kuendeleza maeneo hayo.
Kwa tangazo hili wanapewa siku 14 kuanzia tarehe ya tangazo hili ambayo ni 18 Disemba 2018 wawe wameshaendeleza maeneo waliyopewa na Serikali iweze kukusanya mapato yake.
Aidha kushindwa kufanya hivyo ndani ya siku 14 zilizotolewa itachukuliwa kuwa mhusika hana uwezo na nia ya kuendeleza eneo hilo ,hivyo eneo litachukuliwa na kugawiwa kwa mtu mwingine mwenye uwezo na nia ya kuendeleza.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa