Kuona Majina ya wanafunzi wa Shule za Halmashauri ya Wilaya ya Meru ambao walihitimu darasa la saba mwaka huu 2018 na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2019 Bofya hapa MATOKEO 01.pdf MATOKEO 02.pdfAidha Jumla ya wanafunzi 6766 wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Walifanya mtihani wa kuhitimu darasa la saba mwaka huu 2018, kati yao waliofaulu ni 5825 .
Wanafunzi 4709 kati ya 5825 waliofaulu wamechaguliwa na kupangiwa shule za kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2019.
Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri hiyo Mwl. Sara Kibwana ameeleza kuwa idadi ya wanafunzi 1116 ambao wamebakia wanatarajia kupangiwa hapo badae.
Naye afisa Elimu Sekondari Mwl. Damari Mchome amefafanua kuwa idadi ya Wanafunzi 1116 ambao hawajapangiwa shule watapangwa baada ya miundombinu mashuleni kukamilika (madarasa ).
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa