Sekta ya kilimo ndiyo inayotegemewa kwa kiasi kikubwa na wakazi wa Halmashauri ya Meru, kwani zaidi ya asilimia 75 ya wakazi wa eneo hili wanategemea kilimo kwa ajili ya kuendesha maisha yao ya kila siku.
Halmashauri ya Meru ina Eneo lenye ukubwa wa jumla ya hekta 126,820, kati ya eneo hilo, linalofaa kwa kilimo ni hekta 81,400 ambapo eneo linalolimwa kwa sasa ni hekta 67,931 sawa na asilimia 84 ya eneo lote la kilimo. Vilevile eneo linalofaa kwa umwagiliaji ni hekta 18,745 na linalomwagiliwa kwa sasa ni hekta 12,810. Mkakati uliopo ni kuendelea kufanya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji kadiri bajeti itakavyoruhusu kwa lengo la kuendeleza kilimo cha umwagiliaji. Mazao yanayostawi ni pamoja na; Mahindi, Mpunga, Migomba, Kahawa, Maharage, Maua, Mbogamboga, Matunda, viazi, mihogo, nk.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa