Halmashauri ya Wilaya ya Meru ina vivutio vingi vya Utalii ambavyo vinaweza kuingizia Serikali mapato mengi,vivutio hivyo ni kama vile misitu ya asili iliyofunga yenye wanyama mbali mbali kama vile Mbega weupe,Kima,Tumbili,Dik Dik,Ndege wazuri wa kuvutia pamoja na Wadudu watambaao kama vile Nyoka.Maanguko ya maji,mapango makubwa ya kale,makaburi ya wamisheni wa kwanza Tanzania na eneo maarufu kwa Mila ya Wameru (mringaringa),miti mikubwa ya asili ambayo jamii ya Wameru iliitumia kufanyia matambiko ya kimila.Milima ambayo inatumika kwa shughuli za upandaji (hiking activities) zinaweza fanyika.
Wageni wanapotembelea lodges na hoteli mbali mbali mara nyingi hupata muda mwingi wa kupumzika kabla hawajaendelea na safari zao pindi wanapoingia na baada ya kumaliza safari zao kitu ambacho hupelekea kufanya town or village tourism.Kwa lodge hizi ambazo zinapakana na maeneo vilipo vivutio vya kitalii zitakuwa na fursa ya kufanya ecotourism, walking na utalii wa picha katika maeneo ya Halmashauri kitu ambacho kitaongeza mapato ya Halmashauri.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa