Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro amewataka watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru kuwatumikia wananchi kwa weledi na uaminifu kwa kuzingati Sheria na kanuni za utumishi wa umma kwani Serikali ya awamu ya tano imejikita kutoa huduma bora na zenye viwango kwa Wananchi wake, “tekelezeni majukumu yenu kwa weledi unaojikita katika sheria za utumishi ” amesema Dc. Muro.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema hayo wakati wa kikao na watumishi wa Halmashauri hiyo cha kusikiliza changamoto na kuweka mikakati ya maendeleo kwenye Halmashauri hiyo, na kubainisha kuwa Serikali imekuwa ikitumia kiasi kikubwa cha fedha ili wananchi wake wapate huduma bora hivyo hawana budi kutekeleza majukumu yao “Kwenye Halmashauri hii Serikali inawalipa mishahara zaidi ya Bilioni 43 “amesema Dc. Muro.
Mhe.Jerry Muro amewakumbusha watendaji wa Kata na vijiji kutekeleza majukumu pamoja na kusimamia mapato na fedha zinazotengwa na serikali kwa ajili ya miradi ya maendeleo pia kuhakikisha wafanya biashara kwenye maeneo yao wana leseni za biashara sambamba na kutoa mrejesho kwa wananchi juu ya utekelezaji wa shughuli za Serikali.
Mkuu huyo wa wilaya ameweka bayana hatowavumilia watumishi wasiotekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria lengo likiwa ni kuhakikisha Arumeru inazidi kupata maendeleo kwenye kila Nyanja.
Naye MKurugenzi wa Halmshauri ya hiyo Ndg. Christopher Kazeri akiongea katika kikao hicho ameahidi kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Mhe. Mkuu wa wilaya na kuwasimamia watumishi wa Halmashauri hiyo kutekeleza Majukumu yao.
Kwa upande wa watumishi wa Halmashauri hiyo waliopata fursa ya kuzungumza walieleza wapo tayari kutekeleza majukumu yao na kuiwakilisha vyema Serikali,
Aidha Mkuu wa wilaya ya Arumeru mheshimiwa Jerry Muro, ameanza kazi rasmi ya kuwatumikia wana Arumeru baada ya kuapishwa tarehe 1Agusti 2018.
PICHA ZA TUKIO.
Mhe.Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Baadhi ya wakuu wa idara na watumisi wa Halmashauri ya Meru wakifuatilia kwa makini maelekezo ya Mhe.Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.
Baadhi ya wakuu wa idara na watumisi wa Halmashauri ya Meru wakifuatilia kwa makini maelekezo ya Mhe.Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.
Baadhi ya wakuu wa idara na watumisi wa Halmashauri ya Meru wakifuatilia kwa makini maelekezo ya Mhe.Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa