Waheshimiwa Madiwani na wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Wilayani Arumeru wametakiwa kuzingatia dhana ya mgongano wa maslai katika kutekeleza wajibu wao.
Akizungumza wakati wa Mkutano wa baraza la Halmashauri hiyo kwa siku ya kwanza, Afisa Sekretarieti ya maadili ya Viongozi wa umma, Kanda ya Kaskazini, Ndg.Musiba Magoma kupitia mafunzo ya mgongano wa maslai kwa viongozi wa umma ametoa rai kwa viongozi wa Halmashauri hiyo kuwa waadilifu katika kutekeleza majukumu yao ili kuzitendea haki nafasi walizo nazo na kutoa huduma bora kwa wananchi kwa usawa.
Aidha Musiba amewataka viongozi hao kuepukana na maslai binafsi yenye kuathiri maslai ya umma,ikiwa ni pamoja na kufanya maamuzi yasio na manufaa kwa umma,kutumia rasilimali za Serikali kwa matumizi binafsi, kutumia muda wa kazi kufanya shughuli binafsi sambamba na kutumia madaraka vibaya.
Ndg.Musiba Magoma
Mwenyekiti wa mkutano huo, ambaye pia ni Makamu mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Nelson Mafie amewashukuru Maafisa toka Ofisi ya Rais Sekretarieti ya maadili ya Viongozi wa umma kwa mafunzo ya maswala ya maslai na kuwasihi waheshimiwa madiwani na wataalamu kuzingatia mafunzo hayo.
Mhe.Nelson Mafie Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Meru,
Baadhi ya Waheshimiwa Madiwani wakifuatilia mafunzo ya Mgongano wa maslai kwa viongozi wa Umma.

Baadhi ya Wataalamu wakifuatilia mafunzo ya Mgongano wa maslai kwa viongozi wa Umma.

Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa