Viongozi wa Vijiji 47 vilivyopo kwenye mpango wa kunusuru Kaya maskini kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii ( TASAF) Halmashauri ya Meru Wilayani Arumeru wametakiwa kuwatembelea na kuwahamasisha walengwa wa TASAF toka kaya maskini kuwa na matumizi sahihi ya fedha za ruzuku wanazopokea.
Wito huo umetolewa na mratibu wa TASAF Halmashauri ya Meru,Ndg.Boniface Mwilenga wakati wa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu kwa vikundi vya walengwa wa TASAF katika Kijiji cha Ngyeku Kata ya Kikatiti.
Mwilenga ameeleza kuwa walengwa hao wanapaswa kutumia vyema fedha kwani utekelezaji wa TASAF unalenga kuwawezesha walengwa kujikwamua na kuondokana na hali duni pindi mpango huo utakapo fikia ukomo.
Mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji wa kumbukumbu kwa vikundi vya walengwa wa TASAF yanayo fanyika kwa siku mbili katika kijiji cha Ngyeku na Ngurudoto yatawajengea uwezo wa kujiwekea akiba na kutunzaji kumbukumbu wanachama wapatao 249 toka vikundi 18 wa Vijiji hivyo.
Ikumbukwe kuwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu kwa Wawezeshaji wa TASAF ngazi ya Wilaya na Kata yalifanyika tarehe 25,26,27 Juni 2019,Hivyo kwa sasa wawezeshaji hao wanatoa mafunzo kwa walengwa wakuu wa mafunzo hayo ambao ni vikundi vya walengwa wa TASAF katika vijiji mbalimbali .
Ndg.Hosea Mwankusye ambaye ni Kiongozi wa timu ya wawezeshaji wa TASAF kitaifa akitia saini katika kitabu cha wageni Ofisi ya Mtendaji wa kijiji cha Ngyeku, akiwa ameambatana na Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Meru na wawezeshaji wengine ngazi ya Taifa na Wilaya .
Mwenyekiti wa Kijiji cha Ngyeku Ndg.Elibariki Mungure akitoa ufafanuzi kwa wanachama wa vikundi vya walengwa wa TASAF juu ya ugeni wa wawesheshaji wa TASAF ngazi ya taifa na Wilaya.
Wanachama wa vikundi vya walengwa wa TASAF kijiji cha Ngyeku wakifuatilia mkutano kabla ya Mafunzo
Wanachama wa vikundi vya walengwa wa TASAF kijiji cha Ngyeku wakifuatilia mkutano kabla ya Mafunzo.
Mratibu wa TASAF Halmashauri ya MeruNdg.Boniface Mwilenga akifafanua jambo wakati wa mafunzo katika kikundi kimojawapo cha walengwa wa TASAF kijiji cha Ngyeku.
Ndg.Hosea Mwankusye ambaye ni Kiongozi wa timu ya wawezeshaji wa TASAF kitaifa akiteta jambo na mwenyekiti wa Kijiji cha Ngyeku.
Ndg.Abdallah Dokodoko ambaye mwezeshaji ngazi ya Taifa akizungumza na wanachama wa kikundi kimojawapo cha walengwa wa TASAF Kijiji cha Ngyeku.
Mwezeshaji wa TASAF ngazi ya Wilaya Donatha Minde akitoa mafunzo kwa wanachama wa kikundi kimojawapo kijiji cha Ngyeku.
Mwezeshaji wa TASAF ngazi ya Wilaya akis mafunzo kwa wanachama wa kikundi kimojawapo kijiji cha Ngyeku.
Mwezeshaji wa TASAF ngazi ya Wilaya Sheila akitoa mafunzo kwa wanachama wa kikundi kimojawapo kijiji cha Ngyeku.
Mwezeshaji wa TASAF ngazi ya Wilaya akitoa mafunzo kwa wanachama wa kikundi kimojawapo kijiji cha Ngyeku.
Mwezeshaji wa TASAF ngazi ya Wilaya akitoa mafunzo kwa wanachama wa kikundi kimojawapo kijiji cha Ngyeku.
Mwezeshaji wa TASAF ngazi ya Wilaya akitoa mafunzo kwa wanachama wa kikundi kimojawapo kijiji cha Ngurdoto.
Mwezeshaji wa TASAF ngazi ya Wilaya akitoa mafunzo kwa wanachama wa kikundi kimojawapo kijiji cha Ngurdoto.
Mwezeshaji wa TASAF ngazi ya Wilaya akitoa mafunzo kwa wanachama wa kikundi kimojawapo kijiji cha Ngurdoto.
Mwezeshaji wa TASAF ngazi ya Wilaya Ndg.Getrude Mkumbwa akitoa mafunzo kwa wanachama wa kikundi kimojawapo kijiji cha Ngyeku.
Mwezeshaji wa TASAF ngazi ya Wilaya Lea Linai akitoa mafunzo kwa wanachama wa kikundi kimojawapo kijiji cha Ngurdoto.
Wawezeshaji wa TASAF ngazi ya Wilaya Esta Mbwana(kulia )na Clamentina Mbise wakitoa ufafanuzi wa kina kwa wanachama wa kikundi kimojawapo kijiji cha Ngyeku.
Wanachama wa kikundi kimojawapo kijiji cha Ngurdoto wakifuatilia mafunzo.
Mwezeshaji wa TASAF ngazi ya Wilaya Digna Masawe akitoa mafunzo kwa wanachama wa kikundi kimojawapo kijiji cha Ngurdoto.
Mwezeshaji wa TASAF ngazi ya Wilaya Merry Kiondo akitoa mafunzo kwa wanachama wa kikundi kimojawapo kijiji cha Ngurdoto.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa