Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri Wilaya ya Meru, Ndg.Jonathan Kiama, ametangaza rasmi, majina ya Mipaka ya vijiji vilivyoko katika eneo la halmashauri ya Wilaya ya Meru ambavyo vitahusika katika uchaguzi wa viongozi wa Serikali za mitaa.
Akitangaza Mipaka hiyo, Kiama amesema kuwa, "Kwa Mamlaka niliyopewa chini ya Kanuni ya 5 ya Kanuni ya Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Mji Mdogo Tangazo la Serikali namba 371 la tarehe 26.04.2019 pamoja na Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Wilaya, Tangazo la Serikali namba 373 la tarehe 26.04.2019 na kwa kuzingatia Orodha ya Vijiji na Vitongoji vilivyotangazwa katika Gazeti la Serikali Na 537 la tarehe 19/07/2019.
Msimamizi huyo wa Uchaguzi ametangaza majina ya mipaka halmashauri ya Meru kuwa jumla ya Vijiji 90 na Vitongoji330.
Tangazo hilo ni mchakato kuelekea Uchaguzi wa Serikali za mitaa, unaotegemea kufanyika tarehe 24.11.2019.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa