Watendaji wa Kata na Vijiji Wilayani Arumeru,wametakiwa kuchukua hatua za kudhibiti madawa ya kulevya ikiwemo bangi kama Sheria inavyowataka kwani kutokufanya hivyo ni kujihusisha na kosa la Rushwa kwa matumizi mabaya ya madaraka kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Takukuru Wilaya ya Arumeru Ndg. Deo Mtui baada ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kutoa maagizo ya kusimamishwa kazi kwa Watendaji wa Kata na Kijiji katika Kata ya Mwandeti na Afisa Tarafa wa Mukrati kuwa chini ya uangalizi kwa kushindwa kudhibiti kilimo cha bangi katika maeneo yao
Akizungumza na waendaji hao toka Kata 26 na Vijiji 90,Maafisa Tarafa pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Mkuu huyo wa TAKUKURU amesema kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007 viongozi hao wanapaswa kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya Sheria wale wote wanaotenda uhalifu kwenye maeneo yao ikiwa ni pamoja na uhalifu wa kulima,kuuza na kutumia Bangi.
Mtui ametoa wito kwa viongozi hao kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa Sheria ikiwa ni kuchukua hatua za kudhibiti kilimo cha bangi katika maeneo yao
Mkuu wa Takukuru Wilaya ya Arumeru Ndg. Deo Mtui akizingumza na Watendaji wa Kata na Vijiji ,Wakuu wa Idara na Vitengo Halmashauri ya Wilaya ya Meru .
Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji wakati wa kikao .
Wakuu wa Idara/Vitengo Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakati wa kikao .
Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji wakati wa kikao.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa