• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

JAMII YATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA VYETI VYA KUZALIWA

Imewekwa: May 12th, 2021

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro ametoa wito kwa wazazi/walezi kuchangamkia fursa ya utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5 ikiwa ni kampeni ya Siku 12.

Muro amesema hayo wakati wakati wa ufunguzi wa kampeni ya utoaji vyeti kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5 katika Halmashauri ya Meru uliofanyika katika Hospitali ya Wilaya Tengeru.

Aidha,amesema cheti Cha kuzaliwa kinamanufaa makubwa kwani ni utambulisho rasmi wa Mtoto na takwimu za uandikishaji  zitaisaidia Serekali kufanya mipango ,mikakati na uboreshaji wa huduma za watoto kama vile chanjo,miundombinu sekta ya Elimu nk."Serikali imewasogezea fursa ya vyeti vya kuzaliwa karibu, changamkieni fursa"amehimiza Muro

Muro amewataka Viongozi wa Serikali ,Madiwani, Watendaji wa Kata/ vijiji,Wenyeviti wa vijiji/Vitongoji na Maafisa Tarafa kuhamasisha na kuhakikisha watoto 40263 wa Halmashauri hiyo  ambao ni wanalengwa wanaandikishwa.Pia, ametoa Rai kwa Viongozi wa Dini kuhamasisha jamii juu ya zoezi Hilo.

Mwenyekiti wa Baraza la Halmashauri ya Meru Mhe. Jeremia Kishili ametoa Wito kwa  Madiwani wa Halmashauri hiyokutoa hamasa kwa jamii na wananchi ili wajitokeze kuwaandukisha watoto .

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Dkt. Maneno Focus amesema Wananchi wameitikia zoezi Hilo ambapo kwa siku ya kwanza zaidi ya watoto 950 waliandikishwa.

Bi.Amina ambaye Miongoni mwa wazazi walioandikisha watoto ameishukuru Serikali kwa kusogeza huduma ya vyeti vya kuzaliwa kwa watoto ambayo vinapatikana ndani ya saa chache baada ya kujiandikisha.

IKumbukwe zoezi la utoaji vyeti kwa Watoto chini ya Miaka 5 lilianza rasmi tarehe 11 Mei 2021 katika vituo 79 zikiwa ni ofisi 26 za Kata na vituo 53 vya kutolea huduma za afya.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akikabidhi cheti kwa Mtoto Wakati wa Uzinduzi.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro Akizungumza wakati wa uzinduzi .

Bi.Amina akishuhudi binti take akikabidhiwa cheri acha kuzaliwa wakati wa uzinduzi.

Mganga Mkuu Wilaya Dkt.Maneno Focus akizungumza wakati wa ufunguzi.

Mhe.Jeremia Kishili Mwenyekiti wa Halmashauri ya  Wilaya ya Meru akizungumza wakati wa uzinduzi.

Baadhi ya wakati waliojitokeza wakati wa uzinduzi.

Picha ya pamoja ya Mratibu wa zoezi la utoaji vyeti Bi.Restuta Mvungi(gauni ya njano)wawezeshaji na maafisa waandikishaji wa zoezi la utoaji vyeti kwa watoto chini ya miaka 5.

Siku ya ufungaji mafunzo ya siku 3 kwa waandikishaji wasaidi 

Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • TAHAPAO NA MERU DC WAWEKA NGUVU KWENYE KAMATI ZA MTAKUWA

    February 19, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa