Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Eng.Richard Ruyango ametoa wito kwa makundi mbalimbali wakiwemo ,Wataalamu wa afya,Waalimu,Viongozi wa Vijiji na Vitongoji pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali Wilayani humo kushiriki kikamilifu katika mpango harakishi na shirikishi wa utoaji chanjo ya UVIKO -19 ikiwa ni mapambano dhidi ya ugonjwa huu.
Ruyango amesema hayo wakati wa Mkutano wa Kamati ya Afya ya Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Meru iliyofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Patandi maalumu na kuwajumuisha wadau mbali mbali wa afya.
Aidha,Mhandisi Ruyango amesema kampeni za chanjo dhidi ya magonjwa yanayozuilika zimekua zikifanyika mara kwa mara ambapo kwa sasa Tanzania inaungana nchi nyingine Duniani kuhakikisha inaweka mikakati madhubuti kujikinga na UVIKO -19 ikiwa ni pamoja na utoaji wa chanjo ya ugonjwa huo.
Pia.Ruyango amesema chanjo ya UVIKO-19 inatolewa kwa hiyari katika vituo 55 ndani la Halmashauri ya Wilaya ya Meru pamoja na vituo tembezi ambapo amewataka wadau wa kikao kuwa mabalozi wa kuelimisha umma akitumia kauli mbiu ya "AFYA NI MTAJI,MAPAMBANO DHIDI YA UVIKO -19 NI WAJIBU WETU TUJUMUIKE KWA PAMOJA ,chanjo ni salama".
Vilevile ,Mhandisi Ruyango amewaagiza maafisa wa Tarafa kuhakikisha uhamashishaji wa chanjo unaendelea kupitia mikutano maalumu ili wataalamu wa afya waweze kutoa elimu.
Naye Mhe.Dkt.John D.Pallangyo Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha chanjo ya UVIKO -19 inawafikia wananchi na kutoa wito kwa wabunge kuwa mstari wa mbele kuelimisha na kuhamasisha umma kupata juu ya chanjo UVIKO-19
Mganga Mkuu Halmashauri ya Wilaya ya Meru Dkt.Maneno Focus amesema kirusi cha korona ambacho ni kipya duniani ni sehemu ya familia ya virusi vinavyosababisha homa za mafua kwa miaka mingi hivyo uzalishwaji wa chanjo ya UVIKO-19 umetokana na muendelezo wa tafiti za muda mrefu, juhudi za pamoja kati ya mataifa na dharura ya mlipuko wa ugonjwa.
Aidha Dkt.Focus amewaomba wadau mbalimbali wa afya,Taasisi na sekta mtambuka kushirikiana na idara ya afya ili kufanikisha mpango harakishi na shirikishi wa chanjo ya UVIKO -19 ambapo muitikio wa Viongozi wa Mila ulionekana akiwemo Mshili Mkuu wa Meru Ndg .Hezron Mbise ambaye ameahidi wao kama viongozi wa kimila kutoa elimu kupitia vikao vyao juu ya Chanjo ya UVIKO 19
Kikao hiko kilichojumuisha wadau mbalimbali wa Afya Halmashauri ya Meru kimeazimia kwa kauli moja kufikia lengo la kumaliza chanjo zilizopokelewa kwa asilimia 100 kabla ya mwisho wa mwezi oktoba 2021.
BAADHI YA PICHA ZA TUKIO.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Eng.Richard Ruyango wakati wa kikao na wadau wa afya.
Mganga Mkuu Halmashauri ya Wilaya ya Meru Dkt.Maneno Focus wakati wa kikao na wadau wa afya.
Mhe. Dkt.John D.Pallangyo Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa afya.
Mdau wa EGPAF wakati wa kikao cha wadau wa Afya.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa