Halmashauri ya Wilaya ya Meru Imekabidhi Hundi yenye thamani ya Milioni 93 kwa vikundi 26 vya Wanawake,Vikundi 6 vya Vijana na kikundi kimoja cha watu wenye ulemavu.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango amempongeza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Mkurugenzi Mtendaji, Mhe.Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Waheshimiwa Madiwani na wataalamu kwa usimamizi mzuri wa Halmashauri , kuhakikisha inatoa mikopo kwa Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu Ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Aidha, Ruyango amevitaka vikundi hivyo 33 vilivyopokea Mkopo kuhakikisha vinatumia mkopo kama ilivyokusudiwa kwa Kujiletea maendeleo kupitia Mkopo huo.
Dkt.John D. Pallangyo Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ametoa wito kwa Wafanyabiashara kulipa tozo mbalimbali za Halmashauri kwani fedha hizo hutumika Kuleta maendeleo Jimboni humo,ikiwa ni ujenzi wa Miradi sambamba na kutenga asilimia 10% kuwawezesha kiuchumi Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu.
Mwl.Zainabu Makwinya ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo amewahakikishia Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu kuwa Halmashauri hiyo itaendelea kutoa asilimia 10% za makusanyo yake kwa vikundi hivyo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama (CCM) kilichounda Serikali, Sura ya Pili ibara 23.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe.Jeremia Kishili amesema Madiwani wa Halmashauri hiyo wamejipanga vyema kuhakikisha utoaji wa mikopo kwa Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu unafanyika katika Kata zote 26 kwa kuhamasisha Wananchi na kuwaelimisha juu ya mikopo hiyo.
Aidha Kishili ametoa Wito kwa vikundi vinavyolegalega kurejesha mikopo hiyo kuhakikisha vinarejesha kwa wakati, Ili viendelee kunufaika ikiwa ni pamoja na kuongezewa kiasi Cha mkopo sambamba na kuwezesha Wananchi Wengine kunufaika.
Naye Katibu mwenezi wa CCM Wilaya ya kichama Meru Ndg.Joshua Mbwana amepongeza utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa Vitengo katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru unaolenga kukwamua kiuchumi mwananchi wa Meru.
Mwakilishishi wa UWT,ambaye pia ni Diwani Viti maalum Makiba Mhe.Upendo Salumu ametoa Wito kwa Wanawake kuendelea kuilinda sifa ya mwanamke ya uaminifu kwa kuhakikisha mikopo wanayoipata wanaituma kwa lengo kusudiwa na kurejesha kwa Wakati.
Miongoni kwa Wanufaika wameishukuru Serikali kwa kuweka mazingira nafuu na mepesi ya kuwawezesha Wananchi kiuchumi kwani mikopo hiyo imewawezesha kuongeza Mtaji kupata mahitaji yao ya kilasiku nk.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango wakati wa hafla ya utoaji mikopo.
Dkt.John D. Pallangyo Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki wakati wa hafla ya utoaji mikopo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe.Jeremia Kishili wakati wa hafla ya utoaji Mikopo
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya wakati wa hafla ya ugawaji mkopo.
Katibu mwenezi wa CCM Wilaya ya kichama Meru Ndg.Joshua Mbwana wakati wa hafla ya utoaji mikopo.
Mwakilishishi wa UWT ambaye pia ni Diwani Viti maalum, Makiba Mhe.Upendo Salumu wakati wa hafla ya utoaji mikopo
wanavikundi Wanufaika wa mikopo isiyo na riba, wakati wa hafla ya utoaji mikopo Shilingi Milioni 93.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa