Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa chama cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Humphrey Polepole ameielekeza Halmashauri ya Wilaya ya Meru kuwa wabunifu katika kuwezesha wananchi kiuchumi kwa kuanzisha miradi shirikishi na yenye manufaa kwa wananchi wengi.
Ndg. Polepole ameelekeza hayo alipokua anatembelea kaya za wanufaika wa mpango wa serikali wa kunusuru kaya maskini (TASAF) awamu ya III kwa lengo la kukusanya maoni ya namna ya uboreshaji wa utekelezaji wa TASAF awamu ya nne .
Raeli S. Nasari ambaye ni miongoni mwa wanufaika wa TASAF waliotembele wa wakati wa ziara ya siku moja ya Katibu wa NEC Itikadi na uenezi wa CCM amesema TASAF imebadili maisha yake kwani kwa sasa anamiliki mgahawa mdogo pia ameweza kumsomesha mtoto wake na kuchimba kisima cha maji pamoja na kukarabati nyumba yake.
Aidha ziara hii ya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye Halmashauri hiyo ya Wilaya ya Meru ni muendelezo wa Ziara ya kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwala 2015 – 2020 na kuleta chachu ya kuharakisha kuwahudumia wananchi, kutatua changamoto na kushughulika na shida zao.
Ndg. Humphrey Polepole akizungumza na Elilia Nasari mkazi wa Kata ya King'ori
Ndg.Humphrey Polepole akimpongeza Raeli s. Nasari anayemiliki wa mgahawa
Ndg. Humphrey Polepole akizungumza na Ndekishio Samsoni mkazi wa kijiji cha Sakila Kata ya Kikatiti
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa