Sh.milioni 175,380,000 Kuzinufaisha jumla ya Kaya 5,526 za walengwa wanufaika na mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF) awamu ya III kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru .
Manufaa hayo ni baada ya Serikali kutoa fedha hizo sh.milioni 175,380,000 kama malipo ya mwezi Machi - Aprili kwa walengwa hao 5,526 toka kwenye vijiji 47 vya Halmashauri hiyo ikiwa sh 4,700,000 zitatumika kwa shughuli za usimamizi ngazi ya kijiji.
Boniface Mwilenga ambaye ni Mratibu wa TASAF kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru amesema Halmashauri hiyo kwa kipindi cha kuanzia mwezi Julai 2017 hadi Aprili 2018 imepokea jumla ya sh milioni 854,280,000 kama malipo kwa wanufaika wa TASAF awamu iii.
Mratibu Mwilenga amesema TASAF imefanya mabadiliko makubwa kwenye maisha ya walegwa kwani wengi wao wameboresha makazi pia wamewekeza kwenye shughuli za kuongeza kipato kama vile ufugaji wa mbuzi wa maziwa ,Ng'ombe wa kisasa ,ufugaji kuku pamoja na kujishughulisha na ujasiriamali mdogo mdogo pia baadhi ya walengwa ambao hakuwa na uwezo wa kupata mahitaji kama chakula sasa wanatumia fedha hizo kupata lishe na huduma za afya.
Mmoja wa wanufaika wa utekelezaji wa TASAF awamu ya iii, Rebeca Lazaro mkazi wa kijiji cha Patandi amepongeza uwepo wa mradi huo wa TASAF alio ufananisha na faraja ya mnyonge kwani ukiacha hali duni aliyokuwa nayo,pia ni mjane na familia yake inamtegemea.
Ndg.Richard J. Sumari ambaye ni miongoni mwa wasimamizi (CMC) ngazi ya kijiji akimkabidhi fedha Rebeca Lazaro ambaye ni mnufaika wa TASAF wakati wa malipo kwa kipindi cha Mwezi Machi/Aprili kwenye kijiji cha Patandi.
Ndg.Boniface Mwilenga ambaye ni Mratibu wa TASAF kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa