Wakulima kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru washauriwa kuepuka hasara kwa kutembele na kukagua mazao kwenye mashamba yao mara kwa mara ili kubaini na kumdhibiti kwa wakati mdudu mwaribifu aitwae kiwavijeshi kivaamizi (FALL AMRYWORM) anayeshambulia mimea ya aina 80 mbalimbali kama vile Mahindi,Mtama,Mpunga na uwele .
Akitoa Mafunzo kwa Wakulima wa kijiji cha Nkoasenga Afisa Kilimo Eliudi Saoyo amesema Mdudu huyo Mwaribifu asipo dhibitiwa kwa wakati huwa na Madhara makubwa kwani uharibifu wake huenda kwa hatua kwani huanza kuaribu mmea kwa kushambulia eneo la pembeni la jani na hatua ya pili hushambulia mmea kwa kutoboa jani huku hatua inayofuata ambayo ni vigumu kumdibiti kwani huingia ndani ya mmea ambapo hujitengenezea utando wa kujingika na viatilifu.
Aidha Saoyo amewashauri wakulima hao kuepuka hasara kwa kukagu mashamba yao mara moja na kumdhibiti mdudu huyu kiwavijeshi kivaamizi kwa kutumia kiuatilifu (DAWA) pale wanapo baini uwepo wake pia kutoa taarifa kwa wataalamu wakilimo ili kupata ushauri,
Afisa kilimo Saoyo amesisitiza kuwa matumizi ya viuatilifu ( dawa) hizoo lazima zizingatie vipimo sahihi kwani vipimo visipozingatiwa mdudu huyo hatokufa na kushauri aina ya viuatilifu vinavyoweza kutumika kuwa ni Duduba, Vaashield, Dasban, Duduall, Karate ,Selectroni, Abamecting.
Mwenyekiti wa kijiji cha Nkoasenga Sifael K.Pallangyo ambaye ni miongoni mwa wakulima wa mahindi ambao mashamba yao yameshambuliwa na mdudu huyu Kiwavijeshi mvaamizi amesema"Nilitembelea Shamba langu lenye ukubwa wa Hekari 2.5 nililolima zao la Mahindi na kuona majani yameshambuliwa kwa pembeni hivyo nikapiga dawa mara ya kwanza na yapili bila mafanikio hadi alipokuja Afisa kilimo siku ya Jana na kunielekeza vipimo sahihi ndipo wadudu hawa walikufa".
wakulima wameshukuru kupata elimu hiyo na kuahidi kuitumia pamoja na kuwafikishia wakulima wengine ambao hawakupata pia wameomba Serikali kuwapatia msaada wa viuatilifu (dawa) za kumdibiti mdudu huyo Kiwavijeshi mwaamizi hiyo kwa kudai kuwa viuatilifu hivyo ni vya gharama .
Afisa Kilimo Eliudi Saoyo akiwaelimisha wakulima wa Kijiji cha Nkoasenga juu ya mdudu mwaribifu mazao aitwae Kiwavijeshi kivaamizi (AMRY WORM)
Afisa Kilimo Eliudi Saoyo akiwaonesha wakulima wa Kijiji cha Nkoasenga mojawapo ya kiuatilifu cha kumdhibiti mdudu aitwaye Kiwavijeshi kivaamizi (AMRY WORM)
wakulima wa Kijiji cha Nkoasenga wakifuatilia semina ya mafunzo juu ya mdudu mwaribifu mazao aitwae Kiwavijeshi kivaamizi (AMRY WORM) iliyotolewa na Afisa kilimo Eliud Saoyo.
wakulima wa Kijiji cha Nkoasenga wakifuatilia semina ya mafunzo juu ya mdudu mwaribifu mazao aitwae Kiwavijeshi kivaamizi (AMRY WORM) iliyotolewa na Afisa kilimo Eliud Saoyo.
Mwenyekiti wa kijiji cha Nkoasenga Sifael K.Pallangyo akieleza wakulima wenzake wa kijiji hicho namna alivyogundua uwepo wa mdudu Kiwavijeshi kivaamizi na kumdibiti.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa